Nafasi za Kazi Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar

Maelezo

Chanzo: ZFDA Web



Tarehe Iliyotolewa: 2022-08-16



Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 11642 ... Deadline: 2022-08-19 15:30:00

WAKALA WA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI                            ZANZIBAR

 

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI.

 

Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa chini ya  Sheria Namba 2/2006 na Marekebisho yake Namba 3/2017.

Lengo kuu la kuanzishwa Taasisi hii ni kusimamia Udhibiti wa Usalama na Ubora wa Chakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa vya Utibabu, ili kulinda Afya ya Wazanzibar na watumiaji wa bidhaa hizo kwa ujumla.

Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) inakaribisha maombi ya ajira kwa ajili ya kujaza nafasi katika Ofisi yake ya Unguja kwa waombaji wenye sifa stahiki.

Nafasi zenyewe ni:

  1. AFISA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO (TEHAMA) DARAJA LA II (ZPSG-04), NAFASI 2.

Sifa za Muombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Habari na Mawasiliano (ICT)’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na uzoefu wa kutumia na kusimamia mifumo ya kielektroniki pamoja na miradi mbalimbali inayohusiana na mifumo.
  • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

 

Majukumu:

  1. Kufanya majaribio ya sehemu timilifu za program za Kompyuta (Perform Unit Systems, Module Testing),
  2. Kufanya majaribio ya mifumo ya TEHAMA (Perform E-testing of System Configurations),
  3. Kufanya majaribio ya program za Kompyuta kulingana na mahitaji ya watumiaji (Conducting User Acceptance Test), 
  4. Kuweka usalama wa Vifaa vya TEHAMA ndani ya Taasisi.
  5. Kuzitunza na kuzihakiki taarifa za Taasisi kwa Matumizi ya Serikali.
  6. Kuweka kumbukumbu za miundombinu ya TEHAMA.
  7. Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka.
  8. Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake.

 

  1. DAKTARI MIFUGO DARAJA LA II (ZPSJ-04)(VETERINARY MEDICINE). NAFASI 2.

Sifa za Muombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe amehitimu Shahada ya kwanza ya Udaktari wa Wanyama (Veterinary Medicine) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
  • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

 

Majukumu: 

  1. Kuchunguza na kuzuwia kuenea kwa maradhi ya Mifugo kwa wanyama wanaofikishwa machinjioni.
  2. Kutoa hadhari na hatua za kuchukuliwa kwa maradhi ya miripuko. 
  3. Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka.
  4. Kufanya ukaguzi wa majengo na bidhaa za chakula zinazotokana na mifugo.
  5. Kufanya usajili wa dawa za mifugo.
  6. Kufanya uchunguzi wa bidhaa za chakula zitokanazo na mifugo
  7. Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake

 

 

  1. AFISA TAKWIMU (STATISTICIAN) DARAJA LA II (ZPSG-02) NAFASI 1.

Sifa za Muombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe na shahada ya kwanza ya Statistics, Economics au Commerce kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
  • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

 

Majukumu

  1. Kuendeleza mfumo wa kitaifa wa kukusanya na kuratibu Takwimu za taasisi.
  2. Kukusanya Takwimu pamoja na kuchukua Takwimu za mifano/vielelezo “sampling”.
  3. Kukusanya, kusaidia kuchambua na kuwasilisha Takwimu kwa wakuu wake.
  4. Kusaidia kutengeneza muundo (program) ya kuingiza taarifa za Takwimu katika kompyuta.
  5. Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka.
  6. Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake.

 

 

 

  1. MCHUNGUZI WA VIMELEA (MICROBIOLOGIST) DARAJA LA II (ZPSG-09) NAFASI 1

Sifa za Muombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya “Microbiology” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
  • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

 

Majukumu 

  1. Kufanya chunguzi za sampuli zinazohitaji utaalamu maalum wa kimaikrobiolojia.
  2. Kufanya na kuhakiki matokeo ya uchunguzi wa “microbiology” kwa bidhaa za chakula, dawa na vipodozi.
  3. Kuandaa na kuzifanyia utafiti njia mpya za kufanya uchunguzi wa “microbiology” kwa bidhaa za chakula, dawa na vipodozi.
  4. Kusaidia kutunza vifaa na vitendanishi vya maabara.
  5. Kutunza kumbukumbu za nyaraka na vifaa vya maabara.
  6. Kusaidia kutoa ushauri, kufanya au kushiriki tafiti tofauti na uchunguzi wa sampuli za uhakiki mahiri ( proficiency tests)

 

 

  1. MUHANDISI VIFAA VYA UTIBABU (BIOMEDICAL ENGINEER) DARAJA LA II (ZPSG-09) – NAFASI 1

Sifa za Muombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya “Biomedical Engineering” au “Biomedical Technology” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
  • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

Majukumu

  1. Kuratibu uaandaji wa sifa za vifaa (technical specification), ununuzi, ufungaji (installation), ukarabati, ugezi (calibration) na kuthibitisha vifaa vya maabara.
  2. Kuweza kuthibitisha vifaa vipya kwa kufanya majaribio, kuhakikisha vinafanyakazi kama ilivyotarajiwa na kufanya mabadiliko yanayotakiwa.
  3. Aweze kutoa ushauri kwa uongozi wa maabara kuhusu vifaa vya maabara.
  4. Kutunza vifaa kwa kufanya ukarabati wa awali (preventive maintenance) na kuweka ratiba ya matengenezo.
  5. Kuitisha matengenezo ya vifaa ikiwa ni pamoja na kupitia mikataba ya huduma na kusimamia matengenezo hayo.
  6. Kupokea, kuhifadhi pamoja na kusambaza vifaa vya maabara pamoja na kutunza kumbukumbu.
  7. Kusimamia matumizi sahihi ya vifaa kwa wachunguzi wa maabara ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri wa kitaalam juu ya matumizi bora ya vifaa hivyo.
  8. Kuandaa ripoti ya ufuatiliaji wa vifaa kwa kukusanya, kuchambua na kufupisha taarifa na mwenendo wa vifaa vya maabara.
  9. Kuhakikisha uwepo wa mazingira salama ya ufanyaji kazi kwa kufanya majaribio ya kiusalama (safety test), kushauri na kuafikiana na miongozo, mafunzo na kuwaelekeza wachunguzi kufuata kanuni za kiusalama.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Jinsi ya Kuomba:

 

  • Muombaji anaweza kuwasilisha maombi yake moja kwa moja katika Ofisi ya Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi iliyopo Barabara ya Tomondo (Changu Road), Mombasa Unguja wakati wa saa za kazi.
  • Aidha muombaji anatakiwa aanishe nafasi ya kazi anayoiomba miongoni mwa zilizotajwa hapo juu.

 


Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-

  1. CV ya Muombaji.
  2. Vivuli vya vyeti vya kumalizia masomo na kwa wale waliosoma nje ya nchi, wanatakiwa kuwasilisha vyeti vyao vya uthibitisho kutoka TCU.
  3. Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
  4. Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
  5. Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
  6. N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ au kuomba nafasi zaidi ya moja maombi yake hayatazingatiwa.
  7. Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 19 Agosti, 2022, saa 9:30 Alaasiri.
  8. Barua zote za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

     

 

MKURUGENZI MTENDAJI,
WAKALA WA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR

S.L.P 3595 – ZANZIBAR.

 

Tangazo hili linapatikana pia katika Tovuti ya Taasisi ya Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) ambayo ni Tovuti: www.zfda.go.tz

 



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English