Tangazo la Nafasi za Kazi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar

Maelezo

Chanzo: Utumishi ZanzibarTarehe Iliyotolewa: 2019-05-12Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 15580 ... Deadline: 2019-05-15 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi ya Ualimu wa Shahada ya Kwanza ya Sayansi, Sanaa na Maabara katika Wilaya zifuatazo:-

1.WALIMU WA SHAHADA YA KWANZA SAYANSI - UNGUJA (kwa masomo ya Physics, Mathematics, Chemistry na Biology) a)WILAYA YA KASKAZINI “A” - UNGUJA.

Skuli ni:- Kibeni, Pwani Mchangani, Pale, Tumbatu, Jongowe, Kigunda, Kandwi, Kibuyuni, Kilindi, Kijini, Fukuchani, Bandamaji na Mbuyutendeb)WILAYA YA KASKAZINI “B” - UNGUJA.

Skuli ni:- Makoba, Kilombero, Kiongwe, Bumbwini, Kiwengwa, Upenja, Mgambo na Kitope.
c)WILAYA YA KATI - UNGUJA.

Skuli ni:- Ndijani, Uroa, Jendele, Bambi, Kikungwi, Charawe, Uzi, Umbuji, Chwaka, Ukongoroni, Ubago, Tunguu, Cheju, Dunga, Miwani, Pongwe Pwani na Pongwe Mwera.
d)WILAYA YA KUSINI - UNGUJA.

Skuli ni:- Mtende, Kusini, Muyuni, Michamvi na Muungoni
Sifa za Waombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Ualimu wa Sayansi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.2.WALIMU WA SHAHADA YA KWANZA SANAA - UNGUJA (kwa masomo ya English, Kiswahili, Geography, History na Civics).

SKULI ZINAZOHUSIKA NI:- (Pwani Mchangani, Kigunda, Kibuyuni, Kilindi, Kijini, Fukuchani, Makoba, Mahonda, Cheju, Dunga, Mpapa, Ndijani, Kikungwi, Uzi, Chwaka, Ghana na Bwefum).


Sifa za Muombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Ualimu ya Sanaa kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3.AFISA MAABARA – UNGUJA SKULI ZINAZOHUSIKA NI:- (Mtule, Umoja uzini, Kiembe Samaki “A”, Muanda, Mlimani Matemwe, Faraja na Mpendae).Sifa za Muombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Maabara kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4.WALIMU WA SHAHADA YA KWANZA SAYANSI PEMBA
a)WILAYA YA WETE - PEMBA.

Skuli ni:- Gando, Piki, Kangagani, Uondwe, Chwale, Ukunjwi, Makongeni, Bwagamoyo,Kojani, Mabatini, Kisiwani, Fundo,Mgogoni, Kinyasini na Maziwani.

b)WILAYA YA MICHEWENI - PEMBA.

Skuli ni:- Makangale, Kiuyu, Msuka, Tumbe, Wingwi na Shumba.c)WILAYA YA CHAKE CHAKE - PEMBA

Skuli ni:- Furaha, Chanjamjawiri, Vitongoji, Vikunguni, Mbuzini, Ziwani, Wesha, Pondeani, Kilindi, Pujini, Ndagoni, Uwandani, Kwale, Ole na Mgelema.d)WILAYA YA MKOANI – PEMBA

Skuli ni:- Makoongwe,Wambaa, Mizingani, Ukutini, Chambani, Mtangani, Chwaka, Kiwani, Mkanyageni, Chokocho, Michenzani, Kisiwapanza na Mwambe.Sifa za Waombaji:

•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Ualimu wa Sayansi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Aidha, Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Unguja kwa ajili ya Skuli za Msingi kama ifuatavyo:-

HALMASHAURI YA WILAYA YA KUSINI UNGUJA.

Skuli ni:- Kajengwa Msingi, Muyuni Msingi, Kibuteni Msingi, Muungoni Msingi, Jambiani Msingi, Bwejuu Msingi, Mtende Msingi, Kusini Msingi na Paje Msingi.

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Cheti cha Ualimu wa Sanaa kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Jinsi ya Kuomba:

•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU, TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 -ZANZIBAR.

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi ya kazi pamoja na Skuli anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 15 Mei, 2019 wakati wa saa za kazi.
•Tangazo hili pia linapatikana katika Tovuti www.utumishismz.go.tzShare via Whatsapp
Advertise with us

©2023 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English