Ufadhili wa Masomo M.A Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM)

Maelezo

Chanzo: UDSM WebTarehe Iliyotolewa: 2019-11-07


Download


Kituo cha Kazi/Tukio: UDSM
Imetembelewa mara! 2318 ... Deadline: 2019-11-13 15:00:00

TAASISI YA TAALUMA ZA KISWAHILI

UFADHAILI WA MASOMO YA MA KISWAHILI

 

Taasisi ya Taaluma za Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kampuni ya ALAF Limited inafuraha kuwatangazia ufadhili wa ada kwa wanafunzi watatu (3) wa kusoma Programu ya M.A Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa mwaka wa masomo 2019/2020.

 

Mwaombaji awe na sifa zifuatazo:

 1. Raia wa Tanzania
 2. Mhitimu wa BA Kiswahili
 3. Awe na wakia (GPA) usiopungua 3.8 wa Digrii ya Kwanza
 4. Awe amepata Udahili wa M.A Kiswahili CKD
 5. Umri usiozidi miaka 25
 6. Awe ni muhitaji wa udhamini
 7. Awe na uwezo wa kujigharimia mahitaji mengine (chakula, steshenari, malazi, utafiti n.k)

 

Nyaraka Muhimu za Kutuma

 1. Barua ya maombi ambayo pia itabainisha uwezo wako wa kitaalumma
 2. Nakala ya cheti cha Matokeo ya Kitaaluma ya Shahada ya kwanza (Transcript)
 3. Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa
 4. Maelezo mafupi  (Ukurasa mmoja) kueleza kwa nini unahitaji huo ufadhili

 

Maombi yatumwe kwa:

Ofisi ya Mkurugenzi, 

Taasisi ya Taaluma za Kiswahili

Jengo la Kiswahili, Ofisi Na. 209 AU

Email: iks@udsm.ac.tz

 

Tangazo hili linatangazwa kwa mara ya pili

 

Maombi yatapokelewa kuanzia:

Tarehe 6 Novemba 2019 Mpaka

Tarehe 11 Novemba 2019 

Watakaofanikiwa watajulishwa tarehe 13 Novemba 2019

 

BOFYA HAPA KUPAKUA FAILI LA TANGAZO HILI

 Download

Share via Whatsapp

Advertise a product

©2020 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English