Ni yapi malengo yako kwa mwaka 2023

General Description

Source: Zenjishoppazz



Release date: 2023-01-04



Duty Station: TANZANIA
19704 visits!... Deadline: 2024-10-04 03:23:00

Ni yapi malengo yako kwa mwaka 2023

 

Tukiwa tumeuanza mwaka wa 2023 Miladia, hakikisha unaweka malengo mapya kwa mwaka 2023 ili kupiga hatua mbele, ya Zaidi ulivyopiga katika mwaka 2022.

 

Miongoni mwa mambo ya msingi ni kuhakikisha kwanza unakuwa na nidhamu ya kifedha ambayo itakuwa ndio lengo lako kuu katika kufikikia mafanikio.

 

Pili, usifanye matumizi ambayo hukuyapanga, jambo hili litakufanya kuepuka kununua kila unachokiona, bali utatizama bageti yako inasemaje, jambo hili litakufanya uweze kuwa na akiba ya kutosha katika akaunti yako.

 

Tatu, hakikisha kila siku inayopita huiachi bila ya kujituma sana ili uhakikishe kile siku inayokwenda kwa Mola wake wewe unajituma kwa kufanya kazi na kuweza kuingiza mkwanja hata kama utakuwa ni mdogo.

 

Nne, hakikisha hupotezi pesa hasa kwa matumizi yasio ya msingi, bali tumia kwa malengo na huku Zaidi ukifikiria katika uwekezaji na si katika matumizi ya starehe ambayo gharama yake ni kubwa ambayo kama hujawa makini utakopa madeni ambayo yengeweza kuepukika.



Share via Whatsapp

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2025 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili