Itambue Historia ya Saa

General Description

Source: Zenjishoppazz



Release date: 2023-02-24



Duty Station: TANZANIA
10486 visits!... Deadline: 2025-03-24 06:02:00

HISTORIA YA SAA

 

Saa ni kifaa ambacho hutundikwa, kubebwa au kuvaliwa mkononi ambacho huonesha na kueleza muda husika. Saa tunaweza kuzigawa katika makundi makubwa mawili, nazo ni saa saa za zamani (analog) na saa za kisasa au za dijiti (za kielektroni).

 

Watu waliweza kukisia muda na wakati kwa kutumia jua, tangu dahari na dahari kwa maana miaka mingi hata kabla ya Kristo. Kani miaka ya mwanzoni watu walihesabu saa zao kwa kutegemea mwendo wa jua jinsi inavyoonekana angani na huku wakiangalia kivuli namna kinavyokaa kulingana na mwendo wa jua,  na hapo ndio ikapatikana asili ya saa, kwa kutizama namna kivuli kinavyokuwa kutokana na upande jua linapokuepo.

 

Mbinu nyengine iliyotumiaka ilikuwa kuna chombo ambacho kitaalamu huitwa  (sandglass au sand timer au sand clock au egg timer) chombo hichi hutiwa maji au mchanga, na baadae mchanga huo au maji hayo yanapita ndani ya chombo hicho kutoka juu na kasha kupenya katika shimo jembamba kwenda chini ya chombo hicho. Kutokana na kiwango cha ujazo wa chombo hicho cha chini wakati ulikuwa ukipimwa. 

 

Mifano ya kwanza ya saa hizo za mchanga, inafahamika ya kwamba ilianza kutumika Misri na baadae ikaenea katisa sehemu nyengine za ulimwengu. Hadi leo wapo baadhi ya watu ambao hutumia saa za namna hii katika masuala ya upishi.

 

Mnamo miaka 600 AD zilibuniwa saa zisizotegemea jua au maji lakini pia iliyokuwa na ukubwa pamoja na uzito uliweza kubebeka au kuchukuliwa na mtu mfukoni na kuweza kuibeba kila anapoenda. Inasemekana mwanzoni mwa karne ya 20, saa nyingi zilianza kutumia nishati ya umeme kama vile kwa kuendeshwa kwa kutumia batri kama hizi tunazotumia sasa hivi.

 

Licha ya kwamba matumizi yake siku hizi kuonekana  kupungua kwa kasi hasa kwa vijana kwa sababu kuwepo kwa vifaa vingine ambavyo watu humia kutazama muda, kama simu za mkononi, ambavyo hufanya kazi ya kuonyesha wakati pia kama zilinavyofanya kazi saa za mkononi na ukutani.

 

Dhana ya saa hasa za mkono zina historia ndefu tokea wakati wa uzalishaji wa saa za mwanzo kabisa hasa za mkononi mnamo karne ya 16 AD. Saa hii ilipelekwa kama zawadi kwa Malkia Elizabeth I wa Uingereza kutoka kwa Robert Dudley mnamo mwaka wa 1571.

 

Mwaka wa 1775 iliyoweza kuvalika mkononi na huku mtu akitembea kama namna wanavyotumia watu wengi siku hizi. Saa ya kuvaa mkononi ya zamani kabisa ambayo ipo hadi hivi sasa sasa ni ile ilitengenezwa mnamo mwaka 1806. Miaka ya mwanzoni kabisa, saa za mkono zilikuwa zikivaliwa na wanawake tu, wakati wanaume wao walikuwa wakitumia saa za mfukoni hadi ilipofika karne ya 20 ndipo nao wanaume wakaanza kuvaa mkononi.

 

Saa hizi za mkononi zilianza kuvaliwa na wanaume wanajeshi hadi mwishoni mwa karne ya 19 kwa ajili ya kupanga vyema mipango ya kivita. Kampuni ya Garstin ya London walipewa hati miliki na kampuni ya "Watch Wristlet" mnamo mwaka 1893, lakini walikuwa wakitengeneza saa zenye muundo wa aina kama hizo tangu miaka ya 1880. 

 

Maofisa hao wa Jeshi la Uingereza walianza kutumia saa za mkononi wakati wa kampeni ya kijeshi, ya kikoloni katika miaka ya 1880, Mfano wakati wa Vita vya Anglo-Burma ya 1885.

 

Vita vya Anglo-Burma vilikuwa ni vita kati ya himaya mbili, nazo ni kati ya himaya ya Uingereza dhidi ya Nasabu ya Konbaung, vita hivi vilikuwa miongoni mwa vita vilivyogharimu pesa na mali nyingi Zaidi, na vilivyockhukua muda mrefu hadi kumalizika kwake, na vilipiganwa Kati India na Uingereza, vita hivi viligharimu kati ya pauni milioni 5-13 (pauni milioni 400 hadi bilioni 1.1 kwa mwaka 2019. ) na huchukua zaidi ya miaka 60 hadi kumalizika kwake.

 

Wakati wa mapigano katika vita hivi kulikuwa na umuhimu wa kuratibu harakati zote za vikosi, na kuyasawazisha mashambulizi dhidi ya adui lilikuwa ni jambo muhimu sana, na hapo ndipo matumizi ya saa za mkono yalianza kuenea miongoni mwa maofisa wa kijeshi wa Uengereza. 

 

Kampuni ya Mappin and Webb ilianza uzalishaji wa saa za wanajeshoi huko Sudan mnamo mwaka 1898 na kuongeza kasi ya uzalishaji wakati wa Vita vyake vya pili miaka michache baadaye. 

 

Katika bara la Ulaya kampuni ya Girard-Perregaux na kampuni nyingine za Uswisi zilianza kutengeneza saa za mkononi kwa ajili ya maofisa wa jeshi la Ujerumani mnamo mwaka 1880.

 

Kwa kawaida ubora wa saa unahusishwa kwa kuwepo na mambo mbalimbali kama vile saa zisizoweza kuingia maji (water resistant). Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Usanifishaji wa viwango ulimwenguni  (ISO, the International Organization for Standardization), limetoa vipimo maalum vya saa ambazo haziingi maji, ambapo vigezo hivyo hupambanua zile zinazoingia maji na zile zisizoingia maji. 

 

Hivyo kwa mazingira yetu ya kitanzania ni Bora kununua saa ambazo haziingii maji kwani saa hizo zitaweza kudumu kwa muda mrefu na kutokukufanya ukarudi dukani mara kwa mara kwa kununua kitu hicho hicho na kupoteza pesa ambapo kwenge weza kuepukika.



Share via Whatsapp

Promoted Ads

No preview available
Highheels
114

Visits

TZS 25,000
No preview available
Dishdash
189

Visits

TZS 20,000
No preview available
Night dress
157

Visits

TZS 8,000
No preview available
saa za kike
171

Visits

TZS 15,000
No preview available
vyetezo vya umeme
186

Visits

TZS 10,000
No preview available
maua
84

Visits

TZS 7,000
No preview available
bulb
71

Visits

TZS 3,000

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili