Kutafsiri Sheria, Kanuni na hati nyengine za Kisheria.
Kutoa huduma za kisheria kila inapohitajika.
Kufatilia utekelezaji wa Kanuni na Sheria zinazohusiana na kazi za Mamlaka.
Kuandika na kupitia mikataba, kodi na utoaji wa leseni katika sekta zinazodhibitiwa.
Kupitia rufaa, taratibu na ufuatiliaji wake kisheria.
Kutoa michango katika tafiti za kisheria na musuala mengine ya kisheria ambayo zinazohusiana na Sekta zinazodhibitiwa kulingana na kazi za Mamlaka.
Kuratibu michango na ushauri wa kisheria na kuhusiana na malalamiko yam toa na mpokeaji huduma.
Kuhifadhi kumbukumbu za majadala ya kesi zinazohusiana na Mamlaka.
Kufanyakazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Sifa za Muombaji
Awe ni Mzanzibar mwenye umri usiozidi miaka 45
Awe amehitimu Shahada ya kwanza ya Sheria katika Chuo kinachotambulikana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Kuhusu sheria kwa muombaji wa Fani ya Sheria aliehitimu kuanzia 2019 na kuendelea atalazimika kuwasilisha Cheti cha kuhitimu mafunzo ya Vitendo kutoka Skuli ya Sheria.
Kwa muombaji amehitimu mafunzo yake kabla ya 2019 sio lazima kuwasilisha Cheti cha Mafunzo ya Vitendo.
Wahitimu waliosoma Skuli ya Sheria ya Tanzania au Skuli za Sheria za Nje ya nchi itawalazimu kuwasilisha uthibitisho wa vyeti vyao kuhitimu skuli ya mafunzo ya sheria ya Zanzibar.