Ongeza Spidi ya Computer na Ufanisi wake kwa SSD
General Description
Source: Zenjishoppazz
Release date: 2020-06-19
Ongeza spidi ya computer na Ufanisi wake kwa kuweka disk ya SSD
Kwanini kubadilisha hard disk yako kuwa SSD kutaifanya computer yako kua na speed mara 10 zaidi!!
Hard disk ni kifaa kinachotumika kutunza taarifa (data) katika computer au wakati mwengine katika ‘External hard disk’. Kwa kua kifaa hiki huhifadhi taarifa muhimu zinazohitajika katika utendaji wa computer na mtumiaji wa computer pia, kifaa hiki kina nafasi kubwa katika kuathiri ufanisi wa computer.
Kuanzia mafaili ya windows, applications na mafaili binafsi ya mtumiaji, yote huhifadhiwa kwenye hard disk. Kila wakati mtumiaji anapohitaji kufanya kitendo katika computer, taarifa husomwa au kuhifadhiwa katika hard disk.
Kwa nini hard disk za kawaida zinapunguza spidi ya computer?
Mfumo wa Diski ya Kuzunguka
Hard disk za kawaida (Hard Disk Drives) HDD zina mfumo wa disk ambayo inazunguka ili kusoma au kuweka taarifa, disk inapaswa kuzunguka ili mkono (Spindle) maalumu ambao huandika au kusoma taarifa uweze kufika mahala panapotakiwa na kufanya uandishi au usomaji wa taarifa. Kuzunguka kwa disk Kunachukua muda na pia kunatumia umeme mwingi hivyo kufanya betri kumaliza chaji haraka
Kusoma na kuweka taarifa
Taarifa huwekwa na kusomwa kwa mfumo wa smaku, pia uwezo wa disk hii kusoma na kuandika ni mdogo kwa kipimo cha sekunde. Vile vile kuna wakati disk hizi hufanya kitu kinachoitwa fragmentation, jambo hili hufanya faili moja kuhifadhiwa vipande vipande katika sehem tofauti za disk hivyo kuongeza muda wa kutafuta wakati wa kusoma faili hilo.
Kama Haitoshi
Hard disk hizi
- ni nzito hivyo huongeza uzito wa computer yako,
- lakini pia zikianguka ni rahisi kuharibika na kupoteza data zako.
- Vile vile kutokana na utendaji wake hufanya computer kupata joto (Overheat)
Solid State Drive (SSD)
Hizi di disk ambazo hutumia mfumo wa ki electronic kama ule wa flash disk, badala ya ule wa disk ya kuzunguka. Hivo basi utaratibu huu wa kufanya kazi huwezesha disk hii kufanya kazi kwa speed kubwa Zaidi kwa ufupi disk hizi:
- Zina spidi Zaidi ya mara 10 ya hard disk za kawaida
- Spidi za kusoma na kuandika baina ya 200MB mpaka 550MB kwa sekunde moja wakati Disk za Kawaida ni spidi baina ya 80MB mpaka 160MB kwa sekunde
- Hutumia umeme mdogo hivyo kutunza uhai na utendaji wa betri yako
- Ni nyepesi hivyo kuzifanya Madhubuti hata zikianguka
- Huepusha computer kuwa slow kama vile wakati wa kuwaka au unapofungua mafaili mengi
Kama zilivyo hard disk za kawaida, hizi nazo zipo za ukubwa na makabila tofauti kama vile 128GB, 256GB, 500 GB na makabila Western Digital (WD), Seagate, Kingston na mengineyo.
Jinsi ya Kuzipata
Wasiliana nasi kupata disk hizi pamoja na kuwekewa windows na program kama vile Office, PDF reader, VLC media player na nyenginezo.
Hard disk ya zamani tutaigeuza kuwa External Hard disk ili uweze kuhifadhi mafaili yako mengine.
Wasiliana nasi kwa Whatsapp +255655063601
Others
- Ask Your Self These ten (10) questions
- Jinsi ya kupika Badia (Bagia) za Muhogo
- Dalili za ugonjwa wa moyo ambazo simu yako inaweza kugundua
- Itambue Historia ya Saa
- Jiulize Masuala Haya 10
- 101 Simple Truth for a Better Life
- The Millionaire Fastlane
- The Body Keeps Score
- The Book: The Most Important Thing
- Rich Dad, Poor Dad
- Art of Happiness
- Zanzibar Beaches You Must Visit 2023
- The Millionaire Next Door
- Aina Nne za Watu
- Namna Mazoezi Yanavyosaidia Kuimarisha Tendo La Ndoa
- TIBA ASILIA YA UGONJWA WA BAWASIRI
- Admission Leera Schools
- Vidonda vya Tumbo, Chanzo, Dalili na Tiba Asili za Vidonda vya Tumbo
- Ten Not to miss places to visit in Zanzibar.
- Dawa ya Tonsilis (Matonsisi)
- Jinsi ya ku bold, italic na Kupiga mchoro kwenye Whatsapp
- Dawa ya Bawasiri
- Dawa ya Jino, Tiba Asilia ya Jino linalouma
- Raudhat Medical Clinic
- Jinsi ya kuchagua kompyuta kwa matummizi mbali mbali
- Dawa za asili za pumu
- Dawa za asili zinazootesha nywele na kuzuia upara
- Mahanjumati Makange ya Kuku
- CHOSEN RECIPES EGG CHOP(MINCED MEAT EGG CHOP)