Fursa nzuri kwa wajasiriamali na Wana utafiti

General Description

Source: Zenjishoppazz



Release date: 2017-09-14


Download


Duty Station: Dunia nzima
6493 visits!... Deadline: 2017-12-14 00:00:00

FURSA NZURI KWA WAJASIRI AMALI NA WANA UTAFITI

Kama umeanzisha NGO Shirika Lisilo la kiserikali au una malengo hayo au umeanzisha jambo lolote lile kwa ajili ya kuboresha jamii iliyokuzunguka na ulimwengu kwa ujumla, basi elewa kwamba kuna mashirika mengi duniani ambayo yako tayari kusaidia, kukuza na kuendeleza juhudi za kuboresha hali za watu katika Nyanja tofauti kama vile kipato, afya, kilimo, utawala bora, teknolojia na mengineyo. Mashirika haya hutoa msaada wa kielimu, kifedha, mafunzo na ushauri kwa wahusika na wakati mwengine kugharamia mipango hiyo. Hivyo basi zenjishoppazz imekukusanyia baadhi ya fursa kama hizo ambazo ukifuata maelekezo unaweza ukafaidika na msaada huo. Endelea kusoma hapo chini na ufuate links na maelekezo ili uweze kufanya application, huenda ukawa miongoni mwa watakaofaidika na fursa hizi. Yafuatayo ni maelezo kwa ufupi ya fursa hizo, kwa maelezo Zaidi fuata viunganishi (link) zilizoainishwa hapo chini.

  1. Obama foundation fellowship program 2018 for civic innovators World wide

Obama fellowship inasaidia waanzilishi wa asasi za kijamii ulimwengu mzima katika Nyanja za Sanaa, wajasiri amali, waandishi wa habari ambao wana nia ya kuibadilisha hali ya jamii kuwa nzuri Zaidi. Kwa kuwashawishi raia wenzao katika kuboresha Maisha.

Kwa mara ya kwanza Obama fellowship itafanya mkutano wake April 2018 huko Chicago Marekani na malengo ya mkutano huu wa kwanza pamoja na mafunzo kwa washiriki 20 watakaochaguliwa, itakua ni kuchangia pia katika namna ya kuendesh Fellowship program yenyewe.

Vigezo

  1. Watu wote duniani wanaweza kushiriki
  2. Waombaji lazima wawe na umri kuanzia miaka 18 na kuendeleaa
  3. Wahusika ni wasimamizi, waanzilishi, wanasanaa, wajasiri amali, wanahabari, na wengineo ambao wamo katika taasisi za kiserikali na sekta binafsi.
  4. Wawe wanafanya kazi kwa lengo la kutatua matatizo muhimu katika jamii yao kwa njia za kiufundi na umahiri
  5. Wawe tayari wameonesha mchango wao katika jamii zao na kutambulika kwa jamii kutokana na mchango wao
  6. Wawe na tabia na utamaduni uliokua mzuri pamoja na ustahamilivu
  7. Wawe na uwezo wa kuzungumza Lugha ya kiingereza kwa sababu program itaendeshwa kwa lugha ya kiingereza

Maombi

Maombi yanaweza kufanyika hapa

Kalenda ya Matukio

  1. Ufunguzi wa maombi Jumatano 6, September 2017
  2. Ungwaji wa maombi (Deadline) Ijumaa, October 2017
  3. Majibu ya maombi February 2018
  4. Mkutano wa kwanza wa program April 2018

Program itagharamia safari, viza, na malazi kwa watakaochaguliwa kujiunga.

Kwa masharti, na faida za program hii, na fursa nyengine tembelea tovuti hii

http://opportunitydesk.org/2017/09/07/obama-foundation-fellowship-program-2018/

  1. Afya bora Fellowship

Inahusisha wataalamu wa mambo ya afya na itawafanyia mafunzo washiriki 20 watakaochaguliwa kwa kipindi cha miezi 12. Program itagharamia gharama zote za safari, malazi, chakula ghrama za matumizi za mwezi takriban dola 1500.

Program itawapa wahusika mafunzo yatakayowasaidia kuwa viongozi katika jamii zo kupitia asasi za kiserikali au za kibinafsi au katika taasisi za kielimu.

Tarehe ya mwisho yakuapply ni 1 December 2017

Kwa maelezo Zaidi kama vile vigezo, masharti na namna ya kuapply tembelea kiunganishi hiki

http://opportunitydesk.org/2017/09/07/afyabora-fellowship/

  1. Fuata tovuti hizi kwa fursa nyengine
    1. Wenye sifa na wanaotaka kukuza vipaji vyao vya uongozi. Na ushawishi wao katika kuboresha jamii zao http://www.ngobox.org/fellowship_full-Apply-to-the-IDEX-Fellowship-January-2018-Program-in-India!-IDEX-Accelerator-&-Global-Fellows-Program_4037
    2. Masters na PhD nafasi za FAO http://www.fao.org/fileadmin/user_upload/VA/pdf/IRC4438.pdf



Download

Share via Whatsapp

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili