Islamic Development Bank Fursa ya Masomo ya Elimu ya Juu Shahada ya Kwanza Fani ya Sheria
General Description
|
TANGAZO LA UFADHILI WA MASOMO
Taasisi ya The Islam Development Bank (IsDB) Education Trust Fund Tanzania
Inayo Furaha Kuwatangazia Waislamu Wote Tanzania, Fursa ya Masomo ya Elimu ya
Juu Shahada ya Kwanza Fani ya Sheria
1.0 UTANGULIZI
The Islam Development Bank (IsDB) Education Trust Fund Tanzania ni Taasisi ya Kiislamu iliyosajiliwa na Serikali. Lengo la Taasisi hii ni kusaidia waislamu kujiendeleza katika masuala ya elimu. Katika mwaka wa fedha 2018/2019 IsDB Education Trust Fund Tanzania imeweka malengo ya kutoa MKOPO USIO NA RIBA kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza ya fani ya Sheria - Bachelor of Law. Hivyo, kwa tangazo hili The IsDB Education Trust Fund Tanzania inawaalika vijana wa kiislamu waliohitimu kidato cha sita na kuchaguliwa kusoma shahada ya kwanza ya sheria kwenye vyuo vya hapa nchini kwa mwaka wa masomo wa 2018/19 (wanaoanza masomo mwaka huu) kutuma maombi ya MKOPO USIO NA RIBA kwa kuzingatia mambo yalioelezwa hapo chini.
2.0 MAHITAJI MUHIMU
Ili maombi ya muombaji yaweze kushughulikiwa, yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa:
2.1 Mahitaji ya Kitaaluma
- Muombaji awasilishe barua ya uthibitisho kuwa amedahiliwa katika chuo kimojawapo hapa nchini kusoma shahada ya kwanza ya fani ya Sheria- Bacheler of Law
- Muombaji awe amechaguliwa chuo kwa ufaulu wa kidato cha nne na sita na sio vinginevyo.
- Nakala ya cheti chake cha ufaulu cha kidato cha nne.
- Nakala ya cheti (au result slip) chake cha ufaulu cha kidato cha sita.
2.2 Mahitaji ya Kifedha
Muombaji anatakiwa atoke katika familia yenye mahitaji ya fedha za mkopo na asiwe amepata mkopo toka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania au sehemu nyingine. Hivyo ili kuthibitisha hili muombaji atatakiwa kuwasilisha taarifa zifuatazo katika barua ya maombi itakayotumwa kwa baruapepe:-
- Namba za simu za walimu walezi wa dini ya kiislamu wa kidato cha nne na sita au namba za simu za wakuu wa shule (endapo shule alizosoma hazikuwa na mwalimu mlezi wa dini)
- Nakala ya barua ya utambulisho na uthibitisho wa mahitaji ya kifedha kutoka Jumuiya au Taasisi ya Kiislamu inayomtambua yeye binafsi na familia yake, na inayotambua tabia zake na mchango wake katika jamii kama Muislamu. Barua iwe na jina kamili na namba za simu za viongozi wa Jumuia/Taasisi husika.
2.3 Mahitaji Mengineyo
- Muombaji atume nakala ya cheti cha kuzaliwa kinachoonyesha kuwa amezaliwa sio chini ya mwezi Septemba 1993 (anatakiwa asiwe na miaka zaidi 24 itakapofika Septemba 30, 2018).
- Muombaji awe mtanzania mwenye imani ya kiislamu na mwenye kutekeleza maalekezo ya dini
3.0 Jinsi ya kuwasilisha maombi
Barua ya maombi izingatie mambo yafuatayo;
- Iandikwe kwa kuchapwa kwa lugha ya Kingereza,
- Iwe na majina matatu ya muombaji kama inavyosomeka katika vyeti vyake.
- Iwe na namba ya simu ya mkononi ya mwombaji inayopatikana muda wote,
- Iwe na anuani ya baruapepe ya mwombaji V. Itiwe sahihi ya mwombaji.
- Barua itaje Chuo alichodahiliwa muombaji, na itachukuwa muda gani kuhitimu.
- Barua ya maombi iandikwe kwenda kwa;
The Chairman
IDB Education Trust
P. O. Box 6166
Dar es salaam
Barua ya maombi pamoja na nakala za nyaraka zote zilizotajwa hapo juu zikiwa katika mfumo (Format) ya PDF, zitumwe kwa kupitia anuani ya baruapepe isdbtz2018@gmail.com na nakala yake kwenda kwa lubuva2020@gmail.com,aliamran2012@gmail.com, na ahsakara@hotmail.com kabla ya kupita muda wa ukomo.
Muombaji atumie anuani ya baruapepe yake binafsi au ya mtu mwingine kwa masharti baruapepe husika itumike kutuma taarifa za mtu mmoja tu. Endapo anuani ya baruapepe mmoja itatumika kutuma taarifa zaidi ya mtu mmoja- baruapepe mmoja tu ya kwanza ndiyo itakyopokelewa.
4.0 KIWANGO CHA MKOPO
- Mkopo utahusu maeneo yafuatayo:-
- Fedha za ada ya chuo – itakayolipwa chuoni moja kwa moja
- Fedha za malazi- zitalipwa chuoni/ kwa mwanafunzi menyewe
- Fedha za vitabu-atapewa mwanafunzi mwenyewe
- Fedha za field na utafiti- atapewa mwanafunzi mwenyewe
- Fedha za chakula- atapewa mwanafunzi mwnyewe
- Fedha za gharama za matibabu- zitalipwa chuoni/ kwa mwanafunzi mwenyewe
- Mkopo hautahusu mambo yafuatayo;-
- Gharama za usafiri
- Gharama za usajili
- Matumizi mengine binafsi
5.0 TAREHE MUHIMU ZA KUZINGATIWA
Maombi yatumwe kuanzia |
tarehe 13/09/2018 |
Muda wa ukomo wa maombi |
tarehe 31/10/2018 |
Tangazo Hili Limetolewa na Mwenyekiti wa The Islam Development Bank (IsDB) Education Trust Fund Tanzania