Kozi zilizopewa kipau mbele bodi ya mikopo Zanzibar (ZHELB)

General Description

Source:



Release date: 2017-04-21


Download


Duty Station: Zanzibar
18580 visits!... Deadline: 2017-12-31 00:00:00

BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU ZANZIBAR

FANI ZA VIPAUMBELE WA KIPINDI CHA 2016 - 2020

Tume ya Mipango ya SMZ imetoa taarifa kuhusu utafiti uliofanywa juu ya hali ya utumishi nchini ambayo imeonesha uwepo wa mahitaji makubwa ya wataalamu.

Taarifa hiyo imeibua maeneo ya Vipaumbele vya SMZ juu ya mahitaji ya wataalamu na imeagizwa kuwa taarifa hiyo itumike kama kigezo muhimu kwa utoaji wa mafunzo ya elimu ya juu nchini ili kufikia utekelezaji wa mipango na maendeleo ya rasilimali watu iliyo bora na itakayowaandaa watu wenye ujuzi sahihi, taaluma, tabia na silka zenye tija zinazoendana na mabadiliko ya mfumo wa ushindani wa soko la ajira na kufikia viwango vya juu vya uzalishaji na utoaji huduma.

Ili kurahisisha utekelazaji wa Vipaumbele vya SMZ katika utoaji wa mafunzo ya elimu ya juu, Tume ya Mipango imevigawa vipaumbele hivyo katika madaraja matatu tofauti kulingana na umuhimu wa kila kada kama inavyoonekana katika jedwali la hapo chini.

Hivyo, BMEJZ itazingatia kikamilifu taarifa ya Tume ya Mipango wakati wa upokeaji wa maombi ya mikopo na uteuzi wa waombaji kanzia mwaka wa masomo 2016/17 hadi 2019/20.

TAFADHALI DOWNLOAD FAILI LA PDF HAPO JUU KUPATA ORODHA YA KOZI HIZO.

AHSANTE



Download

Share via Whatsapp

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili