Matekeo ya Mitahani ya Taifa
General Description
Source: BMZ
Release date: 2023-01-21
BARAZA la Mitihani Zanzibar limetangaza matokeo ya darasa la Nne, la Saba na kidato cha pili ambapo matokeo hayo yameonyesha kiwango cha ufaulu kimeongezeka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza hilo, Othman Omar Othman, amesema hayo wakati akitoa taarifa ya matokeo ya mitihani ya taifa ya mwaka 2022 hafla ambayo ilifanyika katika ukumbi wa Wizara ya elimu na mafunzo ya Amali Mazizini mjini Unguja.
Amesema mitihani ya darasa la nne na kidato cha pili ilifanyika kuanzia oktoba 24 mwaka 2022 hadi Novemba 7 mwaka 2022 na kwa mitihan wa darasa la Saba ulifanyika kuanzia Disemba 5 mwaka 2022 hadi Disemba 8 mwaka 2022.
Aidha amesema mitihani hiyo iliendeshwa na kusimamiwa na kamati za uendeshaji wa mitihani za mikoa na wilaya kwa mara ya kwanza kufuatia marekevisho ya sheria Namba 6 ya mwaka 2012.
Amesema ufaulu wa darasa la nne katika mwaka 2022 unaonyesha idadi kubwa ya watahiniwa 25,331 wamefaulu kwa kiwango cha alama D sawa na asilimia 45.11.
"Waliofaulu Daraja C ni 18,943 sawa na asilimia 33.23, Daraja A ni 3,342 sawa na asilimia 5.95 Daraja B ni 2,735 ikiwa sawa na asilimia 4.87 na daraja F ni 5,809 sawa na asilimia 10.34,"amesema
Amesema kwa mwaka 2022 somo la sayansi linaonyesha kuwa na asilimia 97.26 ya watahaniwa waliofaulu huku English ikiwa na ufaulu wa asilimia 88.13.
Mkurugenzi huyo, amesema katika somo la Kiswahili ufaulu ni asilimia 83.17 na Hisabati ni asilimia 72.25.
Pia,amesema watahaniw 160 wenye mahitaji maalum wamefaulu mtihani huo wakiwemo wasioona 3,uoni hafifu 109,viziwi 30,walemavu wa viunho 14 na ulemavu mchanganyiko.
Kwa upande wa matokeo ya darasa la Saba bwana Othman alisema yanaonyesha idadi kubwa ya watahiniwa 18,892 wamefaulu kwa kiwangk cha alama D sawa na asilimia 9.19.
"Watahiniwa waliopata daraja B ni 90 ikiwa sawa na asilimia 0.37 na Daraja F ni 3,339 sawa na asilimia 13.58,"alisema
Amesema katika mwaka 2022 somo la dini limeongoza kwa ufaulu kwa kuwa na asilkmia 92.75.
"Sayansi jamii asilimia 92.27 Kiswahili asilimia 89.04, sanaa,ubunifu na Michezo asilimia 87.64,English asilimia 84.57 science and Technology asilimia 76.22,arab8c asilimia 66.28 na Hisabati asilimia 12.43,"alisema
Pia, Mkurugenzi Othman amesema watahaniwa 53 wenye mahitaji maalum wamefaulu mtihani huo wakiwemo uoni hafifu 36,viziwi 5,walemavu wa viungo 10 na ulemavu mchanganyik 2.
Kwa upande wa matokeo ya kidato cha pili Mkurugenzi huyo alisema kwa mwaka 2022 yameonyesha watahiniwa wengi wamefaulu kwa kupata daraja kwanza 3,893 ikiwa sawa na asilimia 12.09
"Daraja la pili 4,263 sawa na asilimia 13.24 huku daraja la tatu wakiwa 8,793 sawa na asilimia 27.32 na daraja la nne ni 10,639 sawa na asilimi 33.05 pamoja na watahiniwa 4,601 sawa na asilimia 14.30 wamepata divesheni 0,"alisema
Amesema katika mwaka 202 somo la English limeongoza kwa kuwa na ufaulu wa asilimia 94.42, Dini asilimia 94.20.
"Somo la Kiswahili asilimia 93.94,Civics ask miaka 93.10, Geography asilimia 90.12,History asilimia 81.87 na Arabi asilimia 80.30,"alisema
Mkurugenzi huyo alisema somo la chemistry asilimia 78.06, Biology asilimia 74.22, Physics asilimia 56.06 na Mathematics asilimia 22.28.
"Pia watahimiwa 134 wenye mahitaji maalum wamefaulu mtihani huo wakiwemo wasioona 1, uoni hafifu 102,viziwa 20, walemavu wa viungo 10 na ulemavu mchanganyiko 1.
Alisema ufaulu umepanda kwa asilimia 10.81 ukilinganishwa na ufaulu wa asilimia 77.85 wa mwaka 2021.
Akizitaja skuli zilizofanya vizuri kwa upande wa darasala la nne ni skuli ya Great Vision, FEZA, Madrasatul-Ahbaab, Brilliant Academy, Ikh- Las Nursery&Primary, Ali Khamis Camp, Francis Maria na Laureate School Of Zanzibar, Trifonia Academy, Bright Future Academy.
Mkurugenzi huyo, aliwataja watahaniwa 10 bora kitaifa wa darasa la Saba ambaye ni Munir Rashid Ali kutoka skuli ya Hifadhi, Subira Khamis Muhamed kutoka skuli ya Chokocho.
Wengine ni Ismail Yaasin Muombwa kutoka skuli ya Beit-El-Ras, Abdilllah Abdalla Abdillah kutoka skuli ya Kajengwa na Abdalla Mohammed Makame kutoka skuli ya Michenzani.
Mkurugenzi huyo aliwataja wengine ni Mariam Shoka Hamad kutoka skuli ya Konde 'B', Fereji Nasibu Fereji wa skuli ya Mwenge, Rashidi Ally Rashidi wa skuli ya Mtopepo 'B', Ali Juma Othman wa skuli ya Mtopepo 'B' na Hussein Hassan Khamis wa skuli ya ZingweZingwe.
Alisema watahaniwa waliofanya vizuri kitaifa kidato cha pili ni Mustafa Haji Kheir, Raifat Rashid Mussa wa skuli ya Fidelcastro, Fatma Hafidh Mbarouk skuli ya Leera, Suleiman Juka Hamad, Idrisa Juma Hamad, Fatma Amour Mbarouk, Yussuf Salim rashid, Zeyana Ali Othman Abdulwarith Said Suleiman wote wa skuli ya Fidelcastro na Fethal Abdalla Abdillah wa skili ya Hasnuu Makame.
Others
- Ifahamu Museum for the Future Dubai
- Ajali ya MV Spice Islander
- Matokeo ya Kidato cha Nne (Form Four) 2022/2023
- The Motivation Myth
- TABIA 12 ZA MATAJIRI/MAMILIONEA
- Mambo saba ya kujifunza katika kitabu cha The Richest Man in the Babylon
- History Form One Notes
- MAMBO SABA WANAYOYAFANYA MASKINI, AMBAYO MATAJIRI HAWAYAFANYI
- KARIBU USAFIRI NASI KWA SAFARI YA HIJA
- NAMNA NZURI YA KUWEZA KUHIFADHI PESA