AFISA UTAFITI KATIKA SAYANSI YA UVUVI DARAJA LA II - PEMBA - 2 POST
EMPLOYER
WIZARA YA UCHUMI WA BULUU NA UVUVI
APPLICATION TIMELINE:
From: 08-12-2022 To: 22-12-2022
DUTIES AND RESPONSIBILITIES
Kufanya tafiti zinazohusiana na Uvuvi na Sayansi ya Uvuvi
Kuandaa maandiko ya awali (proposal) ya tafiti zinazohusiana na uvuvi na sayansi ya uvuvi
Kuandaa bajeti za tafiti zinazohusiana na sayansi ya uvuvi
Kukusanya taarifa na sampuli za kitafiti za Uvuvi na Sayansi ya uvuvi
Kuandaa ripoti za tafiti anazofanya na zinazofanyika katika Taasisi katika fani yake
Kutoa mrejesho wa tafiti kwa wadau wa uvuvi pamoja na kutoa elimu kwa wavuvi
Kufanya machapisho ya tafiti anazozifanya kwenye Journals zinazotambulika (Peer Review Journals).
Kuandaa ripoti za Utekelezaji wa kazi za kitafiti ikiwemo ripoti ya robo, nusu na ya mwaka
Kuishauri Taasisi juu ya tafiti za Uvuvi na Sayaynsi ya Uvuvi
Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Awe Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka arubaini na sita (46).
Awe amehitimu Shahada ya Pili katika fani ya Sayansi ya Uvuvi (Fisheries Sciences) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Awe na ujuzi wa kufanya Tafiti zinazohusiana na Uvuvi na Sayansi ya Uvuvi
Uzoefu wa kazi pamoja na machapisho za Tafiti katika Journal zinazotambulika (Peer Review Journals) ni sifa za ziada.
Ujuzi wa kuogelea na kuzamia (diving) ni sifa za ziada.