Nafasi za Kazi Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za taifa, MULUWASA na Kwengineko
General Description
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Ref.No.JA.9/259/01/37
08 Septemba, 2021
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Muleba (MULUWASA) na Wizara, Idara Zinazojitegemea na Wakala wa Serikali anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 12 kama zilivyoainishwa hapa chini.
1.0 IDARA YA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA
Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa ilianza kutekeleza shughuli zake kama Idara Inayojitegemea kuanzia mwezi Julai, 2015, ikiwa na maudhui ya Kulinda na Kuhifadhi Urithi andishi wa Taifa letu.
1.0.1 1.0.2
AFISA KUMBUKUMBU II - NAFASI 1
i.
MAJUKUMU YA KAZI
Kudhibiti mifumo ya kumbukumbu, Kutunza na kusimamia matumizi ya kumbukumbu za Wizara, Idara Zinazojitegemea, Vituo vya kutunzia kumbukumbu, Mikoa, Manispaa, Halmashauri za Wilaya, Nyaraka za Taifa na Mashirika ya Umma kulingana na mahali alipo
TAFADHALI PAKUA PDF FILE HAPA KUPATA MAELEZO ZAIDI