Nafasi za Kazi Karume Institute of Technology KIST
General Description
TANGAZO LA KAZI
UTANGULIZI
Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia inatangaza nafasi mbili (02) za kazi kwa nafasi za Uongozi za Manaibu Wakuu wa Taasisi kama ifuatavyo;
1.1 NAIBU MKUU WA TAASISI UTAWALA, MIPANGO NA FEDHA
SIFA ZA MUOMBAJI
1. Awe ni Mzanzibari mwenye kitambulisho cha ukaazi;
2. Awe na Shahada ya Tatu (PhD) katika fani ya Utawala, Uchumi, Sheria na fani yoyote inayolingana na hizo kutoka katika Taasisi inayoyotambulika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
3. Awe na uzoefu wa kiutawala kwa angalau miaka mitatu (03) katika Taasisi ya kitaaluma;
4. Awe na ujuzi wa sheria na sera za kitaifa haswa katika Elimu na Utumishi wa Umma; na
5. Awe na maadili, muadilifu na mweledi kwa kuzingatia katiba ya nchi kuhusu uongozi.
KAZI/MAJUKUMU
1. Atakua Msaidizi Mkuu na Mshauri Mkuu wa Mkuu wa Taasisi katika mambo yote yanayohusiana na utawala, mipango na fedha za Taasisi;
2. Atatekeleza majukumu mengine kama alivyokabidhiwa na Mkuu wa Taasisi kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Taasisi;
3. Kuratibu kazi za Utawala, Mipango na Fedha na Maendeleo katika Taasisi.