Nafasi za Kazi Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar ZAA
General Description
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar, ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa sheria namba 8 ya mwaka 2011. Majukumu ya Mamlaka ya Viwanja Ndege yameelezwa kupitia kifungu nambari 5 (1) ambayo kwa jumla yamejielekeza katika kuviendesha, kuvisimamia, na kuvitunza viwanja vya ndege vya Serikali Unguja na Pemba kwa kuzingatia miongozo ya kitaifa na kimataifa pamoja na kutoa huduma za kuridhisha katika tahadhari (Safety) na usalama (Security) kwa safari za abiria na mizigo katika viwanja vya ndege vya Zanzibar.
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege inatangaza nafasi za kazi 70, katika kada ya kitengo cha Usalama wa kiwanja “Aviation Security” kwa nia ya kuimarisha huduma za Usalama kwa Viwanja vya Ndege vya Unguja na Pemba. Nafasi hizo zitakuwa kwa utaratibu ufuatao