Nafasi za Kazi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Pemba
General Description
Source: Utumishi Zanzibar
Release date: 2018-03-09
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Pemba kama ifuatavyo:-
1. Afisa Sheria Daraja la II “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
2. Dereva Daraja la III “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Cheti cha Udereva na leseni hai class C kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
3. Afisa Maafa Daraja la II “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Usimamizi wa Maafa (Disaster Management) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
4. Muhudumu Daraja la III “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na elimu ya Sekondari na kuhitimu mafunzo ya uhudumu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
5. Afisa Uratibu Daraja la II “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Utawala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
6. Afisa Mipango Daraja la II “Nafasi 2” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Mipango au Uchumi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
7. Afisa Ustawi Daraja la II “Nafasi 1” - Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Ustawi wa Jamii kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.
• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuiainisha nafasi ya kazi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.
Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 14 Machi, 2018 wakati wa saa za kazi.