Nafasi za Kazi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Raisi
General Description
Source: Utumishi Zanzibar
Release date: 2018-10-22
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais kama ifuatavyo:-
IDARA YA MAZINGIRA UNGUJA:
1. Afisa Mazingira Daraja la II “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Sayansi ya Bahari au Mazingira au Usimamizi wa Maliasili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
2. Afisa Mipango Daraja la II “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Mipango au Uchumi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
3. Wasaidizi Afisa Doria Daraja la III “Nafasi 10” Unguja
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata mafunzo ya Ulinzi JKU au JKT.
IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI UNGUJA:
1. Afisa Utumishi Daraja la II “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Rasilimali Watu au Utawala wa Umma kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
2. Afisa Utumishi Msaidizi Daraja la III “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Rasilimali Watu au Utawala wa Umma kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
3. Msaidizi Afisa Utumishi Daraja la III “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Cheti katika fani ya Rasilimali Watu au Utawala wa Umma kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
4. Afisa Habari Daraja la II “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Uandishi wa Habari kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
IDARA YA URATIBU WA SHUGHULI ZA SERIKALI:
1. Afisa Uratibu Daraja la II “Nafasi 2” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Utawala wa Umma au Sheria au Uongozi wa Rasilimali watu au Maendeleo ya Jamii kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
2. Msaidizi Afisa Uratibu Daraja la III “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utawala wa Umma au Sheria au Uongozi wa Rasilimali watu au Maendeleo ya Jamii kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
3. Afisa Habari Msaidizi Daraja la III “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Uandishi wa Habari kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
4. Afisa Utafiti Daraja la II “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Elimu au Utawala wa Umma au Maendeleo ya Jamii kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
5. Afisa Tehama Daraja la II “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya ICT kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
IDARA YA WATU WENYE ULEMAVU UNGUJA:
1. Afisa Walemavu Wilaya Daraja la II “Nafasi 7” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Ustawi wa Jamii au Maendeleo ya Jamii kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
2. Mtunza bustani Daraja la III “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari
IDARA YA MAZINGIRA PEMBA:
1. Afisa Bioanuai Daraja la II “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Biodiversity au Usimamizi wa Maliasili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
2. Afisa Mabadiliko ya Tabia Nchi Daraja la II “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Tabianchi au Usimamizi wa Maliaisili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
3. Mtunza Ghala Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Ununuzi na Ugavi au Uboharia kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
4. Afisa Utumishi Msaidizi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Rasilimali Watu au Utawala wa Umma kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
5. Mwangalizi wa Ofisi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utawala wa Umma au Sayansi ya Jamii au Uongozi wa Rasilimali Watu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
6. Msaidizi Afisa Manunuzi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Ununuzi na Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
7. Katibu Muhtasi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Ukatibu Muhtasi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
8. Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
9. Ulinzi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata mafunzo ya Ulinzi JKU au JKT.
10. Taarishi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari.
11. Afisa Sheria Daraja la II “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
12. Dereva Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata mafunzo ya Udereva
• Awe na leseni hai kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
13. Wasaidizi Afisa Doria Daraja la III “Nafasi 5” Pemba
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata mafunzo ya Ulinzi JKU au JKT.
OFISI YA URATIBU WA SHUGHULI ZA SMZ DAR ES SALAAM:
1. Afisa Utumishi Daraja la II “Nafasi 1” Dar es Salaam
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Rasilimali Watu au Utawala wa Umma kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
2. Afisa Tehama Daraja la II “Nafasi 1” Dar es Salaam
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya ICT kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
3. Afisa Sheria Daraja la II “Nafasi 1” Dar es Salaam
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
4. Afisa Manunuzi Daraja la II “Nafasi 1” Dar es Salaam
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Ununuzi na Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.
• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuiainisha nafasi ya kazi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.
Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 26 Oktoba, 2018 wakati wa saa za kazi.