Nafasi za Kazi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
General Description
Source: Utumishi Zanzibar
Release date: 2018-10-30
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kama ifuatavyo:-
1.Katibu Muhtasi Daraja la III “Nafasi 3”
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashada katika fani ya Ukatibu Muhtasi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
2.Karani Sheria Daraja la III “Nafasi 2”
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
3.Msaidizi Mwangalizi wa Ofisi Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utawala wa Umma au Rasilimali Watu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.
•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.
Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 05 Novemba, 2018 wakati wa saa za kazi