Nafasi za Kazi Shirika la Huduma za Maktaba
General Description
Source: Utumishi Zanzibar
Release date: 2018-10-22
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Shirika la Huduma za Maktaba Unguja kama ifuatavyo:-
1. Ulinzi Daraja la III “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata mafunzo ya Ulinzi JKU au JKT.
2. Taarishi Daraja la III “Nafasi 1” - Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari na kupata cheti
Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.
• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.
Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 26 Oktoba, 2018 wakati wa saa za kazi.