Nafasi za Kazi Skuli ya Sheria Zanzibar
General Description
Source: Utumishi Zanzibar
Release date: 2021-09-15
Skuli ya Sheria Zanzibar (The Law School of Zanzibar (LSZ) ni taasisi iliyoundwa kwa Sheria nambari 13 ya 2019 kwa lengo la kutoa mafunzo bora ya nadharia na vitendo kwa wanasheria na mawakili katika taaluma ya Sheria na fani nyengine zinazohusiana na sheria, vile vile Skuli ya Sheria maendeleo ya kitaaluma ya wanasheria na wahusika wengine katika sekta ya sheria, pamoja na kutoa mchango wa mageuzi ya Sheria na ushauri wa huduma za Sheria kwa jamii.
Skuli ya Sheria Zanzibar inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya kujaza nafasi za Naibu Mkuu wa Skuli - Taaluma na Utawala.
1. Naibu Mkuu wa Skuli - Taaluma (Nafasi Moja (1)
Sifa za Waombaji:
• Angalau awe na Shahada ya kwanza ya Sheria, Utawala, Uchumi au fani inayofanana nazo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na uwezo wa kutumia Kompyuta.
• Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha.
2. Naibu Mkuu wa Skuli - Utawala (Nafasi Moja (1).
Sifa za Waombaji:
• Angalau awe na Shahada ya kwanza ya Sheria, Utawala, Uchumi au fani inayofanana nazo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na uwezo wa kutumia Kompyuta.
• Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha.
MSHAHARA
Mshahara utalipwa kwa mujibu wa viwango vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE
• Awe na uzoefu wa Uongozi usiopungua miaka mitano (5), kati ya hiyo awe ameshafanya kazi angalau miaka mitatu (3) katika nafasi inayofanana na nafasi anayoomba.
• Watumishi walioko katika ajira za Serikali (SMZ) wanaruhusiwa kuomba, na wanatakiwa kupitisha barua zao za maombi kwa wakuu wa taasisi zao.
• Muombaji anatakiwa kuomba nafasi moja tu.
• Ajira ni ya Mkataba wa Miaka Mitatu (3), Baraza linau wezo wa kuteuwa tena na kuongeza muda wa mkataba kwa kipindi kama hicho.
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo ya elimu ya juu
b) Kivuli cha Cheti cha Mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari) na vyeti vyengine vya taaluma.
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Picha nne (4) za “Passport Size” zilizopigwa karibuni.
e) Barua za Maombi ziambatanishwe na Wasifu Binafsi wa Muombaji (CV).
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Barua za maombi ziandikwe kwa mkono na zitumwe kwa utaratibu ufuatao:-
MKUU,
SKULI YA SHERIA ZANZIBAR,
P.O.BOX 3356
MWANAKWEREKWE, (Jengo la Kamisheni ya Utumishi wa Umma)
ZANZIBAR.
Muombaji anatakiwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya SKULI YA SHERIA ZANZIBAR, iliyopo Mwanakwerekwe Zanzibar jirani na Mahakama ya Wilaya, katika Jengo la Kamisheni ya Utumishi wa Umma, wakati wa saa za kazi.
Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni siku ya Ijumaa ya tarehe 24 Septemba, 2021 wakati wa saa za kazi.