Nafasi za Kazi Wizara ya Afya Zanzibar
General Description
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI.
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Afya Zanzibar kama ifuatavyo: -
1. DAKTARI DARAJA LA II (ZPSJ – 09) Nafasi 17 Unguja, Nafasi 8 Pemba.
Sifa za Waombaji:
• Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Tiba ya Binaadamu (Medical Doctor au Medical Doctor and Surgery) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe Mzanzibari
• Awe na vyeti halisi vya kumalizia masomo na cheti cha kuzaliwa.
• Awe na Leseni hai iliyotolewa na Baraza la Madaktari Zanzibar
• Awe na Umri Usiozidi Miaka 46
2. MFAMASIA DARAJA LA II (ZPSG – 09) Nafasi 8 Unguja, 4 Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Ufamasia kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe ni Mzanzibari
• Awe amesajiliwa katika Bodi ya Vyakula na Dawa Zanzibar.
• Awe na vyeti vya kumalizia Masomo na cheti cha kuzaliwa.
• Awe na Umri Usiozidi Miaka 46
3. MTAALAMU WA USINGIZI DARAJA LA II (ZPSG – 09) Nafasi 5 Unguja, 3 Pemba
Sifa za Waombaji:
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya (Bachelor of Science (Medical Science) in “Anesthesia and Critical Care” au Bachelor in Operation Theater and Anesthesia Technology kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe ni Mzanzibari
• Awe na vyeti vya kumalizia Masomo na cheti cha kuzaliwa
• Awe na Umri Usiozidi Miaka 46
4. MTABIBU AFYA YA AKILI (MENTAL HEALTH AND REHABILITATION) DARAJA LA II (ZPSG – 09) Nafasi 1 Unguja 1 Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya “Mental Health and Rehabilitation” au “Clinical Rehabilitation Counseling au Rehabilitation and Disability/Clinical Psychology and Rehabilitation/Clinical Psychiatric and Rehabilitation kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe ni Mzanzibari
• Awe na vyeti vya kumalizia Masomo na cheti cha kuzaliwa
• Awe na Umri Usiozidi Miaka 46
5. DAKTARI BINGWA WA WATOTO (DOCTOR OF MEDICINE IN PADIATRICS) DARAJA LA II (ZPSK – 09) Nafasi 1 Unguja.
Sifa za Waombaji:
• Awe amehitimu Shahada ya Pili katika Fani ya Utabibu wa Watoto (Master of Medicine in Pediatrics) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe na Uzoefu Usiopungua Mwaka Mmoja katika tasniya ya Utabibu katika Ngazi ya Shahada ya Kwanza.
• Awe na Leseni hai kutoka Baraza Husika
• Awe ni Mzanzibari
• Awe na vyeti vya kumalizia Masomo na cheti cha kuzaliwa
• Awe na Umri Usiozidi Miaka 46
6. AFISA USIMAMIZI MIRADI, UFUATILIAJI NA TATHMINI KATIKA AFYA DARAJA LA II (ZPSG – 8) Nafasi 1 Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe amehitimu Shahada ya Pili ya Usimamizi Miradi, Ufuatiliaji na Tathmni katika Afya (Project Management, Monitoring and Evaluation in Health) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe Mzanzibari
• Awe na vyeti halisi vya kumalizia masomo na cheti cha kuzaliwa.
• Awe na umri usiozidi miaka 46
7. AFISA MSIMAMIZI MIFUMO YA AFYA DARAJA LA II (ZPSG-09) Nafasi 1 Unguja, 1 Pemba.
Sifa za Waombaji:
• Awe Amehitimu Shahada ya Kwanza ya usimamizi wa Mifumo ya Afya (Health Information System/ Health Management System / Health Informatics) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe Mzanzibari
• Awe na vyeti halisi vya kumalizia masomo na cheti cha kuzaliwa.
• Awe na umri usiozidi miaka 46
8. AFISA LISHE DARAJA LA II (ZPSG – 09) Nafasi 7 Pemba.
Sifa za Waombaji:
• Awe amehitimu Shahada ya kwanza ya Lishe, Sayansi Kimu na Lishe au Sayansi ya Chakula na Teknolojia ya Chakula (BSc – Nutrition au Home Economics and Nutrition au Food Science and Technology au Food Science) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe Mzanzibari
• Awe na Vyeti halisi ya kumalizia masomo na cheti cha kuzaliwa.
• Awe na umri usiozidi miaka 46
9. DAKTARI WA KINYWA NA MENO DARAJA LA II (ZPSJ – 09) Nafasi 01 Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Tiba ya Meno (Medicine/Dental) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe Mzanzibari
• Awe na vyeti halisi vya kumalizia masomo na cheti cha kuzaliwa.
• Awe amemaliza mafunzo ya vitendo (Internship) kwa muda wa mwaka mmoja katika hospitali zilizoteuliwa na Serikali.
• Awe amesajiliwa katika Baraza la Madaktari Zanzibar.
• Awe na Leseni hai ya Baraza la Madaktari Zanzibar.
• Awe na umri usiozidi miaka 46
10. AFISA TABIBU MENO DARAJA LA III (ZPSF – 01) Nafasi 5 Unguja, 5 Pemba.
Sifa za Waombaji:
• Awe amehitimu Stashahada ya utabibu Meno (Dental Therapist) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe ni Mzanzibar
• Awe na leseni hai ya Utabibu kutoka Baraza la Madaktari Zanzibar.
• Awe na Chet halisi cha Kumalizia Masomo na cheti cha Kuzaliwa.
• Awe na umri usiozidi Miaka 46
11. MHANDISI VIFAA TIBA DARAJA LA II (ZPSG – 09) Nafasi 2 Unguja, 1 Pemba.
Sifa za Waombaji
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Uhandisi Vifaa Tiba (Biomedical Engineering) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na Chet halisi cha Kumalizia Masomo na Cheti cha Kuzaliwa.
• Awe na umri usiozidi Miaka 46
12. FUNDI SANIFU VIFAA TIBA DARAJA LA III (ZPSF – 01) Nafasi 4, Unguja 02 Pemba.
Sifa za Waombaji:
• Awe amehitimu Stashahada ya Vifaa Tiba (Biomedical Technician ) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali
• Awe ni Mzanzibari
• Awe na Chet halisi cha Kumalizia Masomo
• Awe na umri usiozidi Miaka 46
13. MFIZIOTHERAPIA DARAJA LA II (ZPSG – 09) Nafasi 5 Unguja.
Sifa za Waombaji:
• Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Fiziotherapia (Physiotherapy) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe ni Mzanzibari
• Awe na Vyeti halisi vya kumalizia Masomo na Cheti cha Kuzaliwa.
• Awe na umri usiozidi miaka 46
14. MFIZIOTHERAPIA DARAJA LA III (ZPSF – 01) Nafasi 03 Pemba.
Sifa za Waombaji:
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Fiziotherapia (Physiotherapy) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na Vyeti halisi vya kumalizia Masomo na Cheti cha Kuzaliwa.
• Awe na umri usiozidi miaka 46
15. SONOGRAPHER DARAJA LA III (ZPSF – 01) Nafasi 8 Unguja, 3 Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe amehitimu Stashahada ya Medical Imaging kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali
• Awe Mzanzibari
• Awe na vyeti halisi vya kumalizia masomo na Cheti cha Kuzaliwa.
• Awe na umri usiozidi miaka 46
16. MHANDISI UMEME DARAJA LA II (ZPSG – 08) Nafasi 2 Unguja, 1 Pemba .
Sifa za Waombaji:
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Uhandisi wa Umeme kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe Mzanzibari
• Awe na Vyeti halisi vya Kumalizia Masomo na Cheti cha Kuzaliwa.
• Awe na umri usiozidi miaka 46
17. BIOSTATISTICIAN DARAJA LA II (ZPSG – 09) Nafasi 2 Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe mwenye Shahada ya kwanza ya Bio-statistics kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe Mzanzibari
• Awe na vyeti halisi vya kumalizia masomo
• Awe na umri usiozidi miaka 46
18. AFISA SHERIA DARAJA LA II (ZPSG – 08) Nafasi 1 Pemba.
Sifa za Waombaji:
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Sheria kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe Mzanzibari
• Awe na Vyeti halisi vya kumalizia Masomo na Cheti cha Kuzaliwa.
• Awe na Umri Usiozidi Miaka 46
19. OPTOMETRIST DARAJA LA II (ZPSG– 09) Nafasi 2 Unguja.
Sifa za Waombaji
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza (Optometry/Ophthalmology kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na Vyeti halisi vya kumalizia masomo na Cheti cha Kuzaliwa.
• Awe na umri usiozidi miaka 46
20. OPTOMETRIST DARAJA LA III (ZPSF – 01) Nafasi 3 Unguja.
Sifa za Waombaji
• Awe na Stashahada ya (Optometry/Ophthalmology kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na Vyeti halisi vya kumalizia masomo na Cheti cha Kuzaliwa.
• Awe na umri usiozidi miaka 46
21. AFISA USHAURI NASAHA DARAJA LA II (ZPSG – 09) Nafasi 4 Pemba.
Sifa za Waombaji:
• Awe mwenye Shahada ya Kwanza ya Ushauri Nasaha kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe Mzanzibari
• Awe na Vyeti halisi vya kumalizia Masomo
• Awe na umri usiozidi miaka 46
22. SYSTEM DEVELOPER DARAJA LA II-(ZPSD – 01) Nafasi 5 Unguja.
Sifa za Waombaji
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Kompyuta (Computer Science), au “Software Engineering” au Computer Engineering kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe ni Mzanzibari
• Awe na vyeti halisi vya kumalizia masomo na checti cha kuzaliwa.
• Awe na umri usiozidi miaka 46.
• Awe na uwezo wa kutumia na kutengeneza mifumo ya kompyuta ya Taasisi kwa kutumia programing language kama C++, Java Script, Java, PHP, Oracle na MySql program, laravel, node, python angular & react na spring boot.
23. CIVIL ENGINEER DARAJA LA II-(ZPSD – 01) Nafasi 4 Unguja, 2 Pemba.
Sifa za Waombaji
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya “Civil Engineering” au “Structural Engineering” au “Architectural Engineering” kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe ni Mzanzibar
• Awe na vyeti halisi vya kumalizia masomo na cheti cha kuzaliwa.
• Awe na Umri usizidi miaka 46
24. AFISA MANUNUZI NA UGAVI DARAJA LA II(ZPSG–08) Nafasi 2 Unguja .
Sifa za Waombaji:
• Awe amehitimu Shahada ya kwanza ya Manunuzi na Ugavi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe Mzanzibari.
• Awe na vyeti halisi vya kumalizia masomo na cheti cha kuzaliwa.
• Awe na Umri usizidi miaka 46
25. AFISA MIPANGO DARAJA LA II (ZPSG – 08) Nafasi 1 Pemba .
Sifa za Waombaji:
• A we amehitimu Shahada ya kwanza ya Mipango (Planning) au Uchumi (Economics) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe Mzanzibari
• Awe na vyeti halisi vya kumalizia masomo na cheti cha kuzaliwa.
• Awe na Umri usizidi miaka 46
26. AFISA MIRADI DARAJA LA II (ZPSG – 08) Nafasi 2 Unguja.
Sifa za Waombaji:
• Awe amehitimu Shahada ya kwanza ya Usimamizi wa Miradi (Project Management) au Uchumi (Economics) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe Mzanzibari.
• Awe na vyeti halisi vya kumalizia masomo na cheti cha kuzaliwa.
• Awe na Umri usizidi miaka 46
27. FUNDI AC DARAJA LA III (ZPSE – 10) Nafasi 1 Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe amehitimu Astashahada (elimu ya cheti) ya “Air Condition and Refrigeration” kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na vyeti halisi vya kumalizia masomo cha kuzaliwa.
• Awe na umri usiozidi miaka 46
28. DEREVA DARAJA LA III (ZPSF – 01) Nafasi Nafasi 11 Unguja, 04 Pemba.
Sifa za Waombaji:
• Awe amehitimu Kidato cha Nne (F – IV) na kupata cheti.
• Awe na Leseni hai ya dereva Daraja la B1au D1 inyotambuliwa na Serikali.
• Awe ni Mzanzibar
• Awe na vyeti halisi vya kumalizia masomo na cheti cjha kuzaliwa.
• Awe na umri usiozidi miaka 46
Jinsi ya Kuomba:
• Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya Kielektroniki kwenye mfumo wa
Maombi ya Ajira (Zan-Ajira) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.zanajira.go.tz kuanzia tarehe 5 Agosti, 2024 hadi tarehe 16 Agosti, 2024.
• Tangazo hili pia linapatikana katika tovuti ya Tume ya Utumishi Serikalini www.zanajira.go.tz
• Barua za maombi zitumwe kwa anuani ifuatayo kupitia mfumo wa ZanAjira (kwa njia ya kielektroniki pekee): -
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S.L.P 1587,
ZANZIBAR
• Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi ya kazi anayoiomba.
• Muombaji atakaewasilisha “Progressive Report” au “Statement of Results” pekee maombi yake hayatazingatiwa.
• Kwa msaada wa kitaalamu wasiliana na Tume ya Utumishi Serikalini kupitia e-mail helpdesk@zanajira.go.tz au simu Nam. 0773101012
AHSANTENI