Nafasi za Kazi Wizara ya Elimu
General Description
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na. JA.9/259/01/A/199 22 Disemba, 2022
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizaraya Elimu, Sayansi na Teknolojia anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi ishirini na tano (25) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.
1.0 MWAJIRI: WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
1.1 MKUFUNZI MSAIDIZI MAENDELEO YA JAMII II (UMEME) - NAFASI 15
1.1.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kufundisha masomo ya fani ya Umeme katika Vyuo;
Kuandaa mitiririko na mpangilio wa masomo;
Kusimamia masomo ya vitendo;
Kuwapima wanachuo wakati wa mazoezi na kwenye mitihani;
Kufanya utafiti wa mahitaji ya mafunzo katika Jamii inayozungukachuo; Kuandaa muhtasari wa masomo;
Kufanya maandalizi ya namna ya kuendesha mafunzo; Kuandaa vielelezo vya kufundishia;
Kuendesha mafunzo ya nje ya Chuo (Outreach Programs); na
1
x. Kutunga, Kusimamia na Kusahihisha mitihani.
1.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne/sita waliofuzu mafunzo ya Stashahada kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika fani ya umeme
1.1.3 MSHAHARA:
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C
1.2 MKUFUNZI MSAIDIZI MAENDELEO YA JAMII II (MAGARI) - NAFASI 10
1.2.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kufundisha masomo ya fani ya Magari katika Vyuo;
Kuandaa mitiririko na mpangilio wa masomo;
Kusimamia masomo ya vitendo;
Kuwapima wanachuo wakati wa mazoezi na kwenye mitihani;
Kufanya utafiti wa mahitaji ya mafunzo katika Jamii inayozunguka chuo;
Kuandaa muhtasari wa masomo;
Kufanya maandalizi ya namna ya kuendesha mafunzo;
Kuandaa vielelezo vya kufundishia;
Kuendesha mafunzo ya nje ya Chuo (Outreach Programs); na
Kutunga, Kusimamia na Kusahihisha mitihani.
CLICK HERE TO DOWNLOAD PDF FILE FOR MORE INFORMATION