Nafasi za Kazi Wizara ya Fedha na Mipango

General Description

Source: Utumishi Zanzibar



Release date: 2018-10-22



Duty Station: Zanzibar
1149 visits!... Deadline: 2018-10-26 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Wizara ya Fedha na Mipango kama ifuatavyo:-

IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI:
1. Afisa Utumishi Daraja la II “Nafasi 3” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Rasilimali Watu au Utawala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

2. Dereva Daraja la III “Nafasi 2”
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata mafunzo ya Udereva
• Awe na leseni hai kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Mtunza Kumbukumbu Daraja la III “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada ya Kutunza Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. Programmer wa Computer Daraja la II “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Programme ya Computer kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. Mtunza Ghala Daraja la III “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada ya Kutunza Ghala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6. Afisa Ununuzi na Ugavi Daraja la II “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Ununuzi na Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar


7. Taarishi Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Muombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari.

IDARA YA FEDHA ZA NJE:

8. Afisa Uhusiano Daraja la II “Nafasi 2” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya ‘Law in International Relation’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

9. Afisa Uchumi Daraja la II “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uchumi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

IDARA YA MITAJI YA UMMA:

10. Afisa Mtathmini wa Ardhi Daraja la II “Nafasi 3” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Uongozi wa Ardhi (Land Management and Valuer) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

OFISI YA MUHASIBU MKUU WA SERIKALI:

11. Muhasibu Daraja la II “Nafasi 2” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Uhasibu’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuiainisha nafasi ya kazi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 26 Oktoba, 2018 wakati wa saa za kazi.



Share via Whatsapp

Others

Promoted Ads

No preview available
Highheels
566

Visits

TZS 25,000
No preview available
Dishdash
366

Visits

TZS 20,000
No preview available
Night dress
344

Visits

TZS 8,000
No preview available
saa za kike
387

Visits

TZS 15,000
No preview available
vyetezo vya umeme
359

Visits

TZS 10,000
No preview available
maua
277

Visits

TZS 7,000
No preview available
bulb
204

Visits

TZS 3,000

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili