Nafasi za Kazi Wizara ya Ujenzi , Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar

General Description

Source: Utumishi Zanzibar



Release date: 2018-11-05



Duty Station: Zanzibar
13682 visits!... Deadline: 2018-11-09 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji kama ifuatavyo:-

IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI-UNGUJA

1.Afisa Utawala Daraja la II “Nafasi 1” Unguja

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Public Administration kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


2.Fundi Umeme Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Ufundi wa Umeme kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3.Walinzi Daraja la III “Nafasi 2” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amemaliza elimu ya Sekondari.
•Awe amepata mafunzo ya Ulinzi (Mgambo au JKU au JKT)

4.Mpiga Picha Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Upigaji picha kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


IDARA YA USAFIRI NA LESSENI – UNGUJA

1.Afisa Manunuzi Daraja la II “Nafasi 1” Unguja

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Manunuzi na Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Afisa Upasishaji Daraja la III “Nafasi 1” Unguja

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Ufundi Magari (Mechanic) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


IDARA YA UJENZI NA UTUNZAJI WA BARABARA

1.Afisa Manunuzi Daraja la II “Nafasi 1” Unguja

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Manunuzi na Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2.Mtunza Ghala Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Kutunza Ghala (Material Management) au Manunuzi na Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

3 Fundi Umeme Magari/Mitambo (Auto Electrical) Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Ufundi wa Umeme Magari au Mitambo (Auto Electrical) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.



IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI – PEMBA

1.Walinzi Daraja la III “Nafasi 2” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amemaliza elimu ya Sekondari.
•Awe amepata mafunzo ya Ulinzi (Mgambo au JKU au JKT).



IDARA YA USAFIRI NA LESENI - PEMBA

1.Fundi Welding Daraja la III “Nafasi 2” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Ufundi Welding kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2.Fundi Magari Daraja la III “Nafasi 2” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Ufundi Magari (Mechanics) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 09 Novemba, 2018 wakati wa saa za kazi.
 



Share via Whatsapp

Others

Promoted Ads

No preview available
Highheels
566

Visits

TZS 25,000
No preview available
Dishdash
366

Visits

TZS 20,000
No preview available
Night dress
344

Visits

TZS 8,000
No preview available
saa za kike
387

Visits

TZS 15,000
No preview available
vyetezo vya umeme
359

Visits

TZS 10,000
No preview available
maua
277

Visits

TZS 7,000
No preview available
bulb
204

Visits

TZS 3,000

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili