Nafasi za Masomo (Scholarships) SMZ
General Description
Tangazo la Nafasi za Masomo Kupitia Ufadhili Wa Benki Ya maendeleo ya kiislamu
Bodi ya mikopo ya elimu ya juu zanzibar (bmejz) inatangaza nafasi za masomo ya shahada ya kwanza kupitia ufadhili wa serikali ya mapinduzi zanzibar kwa mwaka wa masomo 2018/19.
Waombaji wa nafasi hizo wanatakiwa wawe na sifa zifuatazo:
- Wawe wamemaliza kidato cha sita mwaka 2018 na kupata ufaulu wa daraja la kwanza katika masomo ya sayansi.
- Wawe na umri usiozidi miaka 22 ifikapo septemba 2018.
- Wawe na afya njema.
- Wawe wazanzibari.
Barua za maombi ziambatanishwe pamoja na:
- Vivuli vya vyeti vya masomo na matokeo ya mitihani ya kidato cha nne na kidato cha sita .
- Kivuli cha kitambulisho cha mzanzibari.
- Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
Fomu za maombi zinapatikana katika ofisi za bodi ya mikopo ya elimu ya juu zanzibar zilizopo vuga unguja na chakechake pemba.
Muda wa mwisho wa kurejesha fomu za maombi zilizojazwa kikamilifu ni tarehe 17 agosti, 2018.
IMETOLEWA NA MKURUGENZI, BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR.