Nafasi za Masomo Al Azhar University Misri

General Description

Source: MOEZ



Release date: 2019-05-13



Duty Station: Egypt
8299 visits!... Deadline: 2019-06-24 15:30:00

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR INATANGAZA NAFASI ZA MASOMO SHAHADA YA KWANZA YA PILI NA YA TATU NCHINI MISRI KATIKA CHUO CHA “AL-AZHAR” KWA MWAKA WA MASOMO 2019/2020.

FANI ZINAZOTOLEWA NI ZA ART NA SCIENCE AMBAZO NI:

  • ECONOMIC AND POLITICAL SCIENCE,
  • INFORMATION,
  • DENTISTRY,
  • VETERINARY MEDICINE,
  • ARCHEOLOGY,
  • SCIENCE,
  • PHYSICAL EDUCATION,
  • HUMANITY SCIENCES,
  • EDUCATION,
  • TOURISM AND HOTELS,
  • NURSING,
  • APPLIED ARTS,
  • FOUNDATION OF EDUCATION,
  • LITERATURE,
  • BUSINESS,
  • CHILD SPORTS,
  • SCIENCE (YOUNG WOMAN),
  • LITERATURE (YOUNG WOMAN),
  • FINE ARTS,
  • RIGHTS,
  • EDUCATION (CHILDHOOD),
  • AGRICULTURE,
  • ENLIGHTENMENT / EDUCATION,
  • HOME ECONOMY,
  • EDUCATION/ PART OF SCIENCE (YOUNG WOMAN),
  • EDUCATIONAL GYMNASTICS,
  • EDUCATIONAL ARTS (YOUNG WOMAN).
  •  

SIFA ZA MUOMBAJI

 

  • Muombaji awe Muislam
  • Awe hajawahi kuomba nafasi hii na kuteuliwa kisha akaipoteza kwa sababu yoyote ile.
  • Asiwe na maradhi ya kudumu au kuambukiza.
  • Asiwe ameteuliwa kaika sehemu nyengine ndani ya Misri au kwengineko.
  • Fomu zote zinazohitajika zikamilike na ziwe zimegongwa muhuri katika Ubalozi wa Misri kabla ya kupelekwa. Sambamba na hayo, fomu ziandikwe kwa lugha ya Kiarabu, au Kiingereza au Kifaransa, au zitafsiriwe kwa moja ya lugha hizo tatu.
  • Jina la Mwanafunzi liende sambamba na majina yaliyo katika vyeti vyake vyote vinavyotakiwa kuambatanishwa.
  • Mwanafunzi anaweza kubadilishwa kutoka kitivo alichoteuliwa kwenda kitivo chengine mara moja tu kukiwa na haja hiyo.
  • Chuo kitampatia Mwanafunzi tiketi ya kurudi kwao akimaliza masomo na akiwa amefaulu.
  •  

NJIA YA KUFANYA MAOMBI

 

Fomu za maombi zinapatikana Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, katika Kitengo cha Uratibu wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia chumba namba 57. Baada ya kukamilika kwa fomu hizo ziwasilishwe chumba namba 57 zikiambatanishwa na vitu vifuatavyo:-

  • Vivuli vya vyeti vya kumaliza masomo, vigongwe muhuri wa Wizara ya mambo ya Nchi za nje wa Tanzania na Ubalozi wa Misri ulioko Tanzania.
  • “Statement of result” za masomo aliyohitimu na kupata vyeti hivyo. (ziwe zimegongwa muhuri).
  • Kivuli cha cheti cha kuzaliwa kilichogongwa muhuri wa Wizara ya mambo ya Nje ya Tanzania na ya Ubalozi wa Misri.
  • Picha sita za paspoti (mpya) nyuma ziandikwe jina lake na utaifa wake.
  • Kivuli cha pasi ya kusafiria ambayo imeshasafiriwa.
  • Tazkia kutoka katika Taasisi zinazokubalika.
  • Barua kutoka Ubalozi wa Misri uliopo Nchini.
  • Fomu ya uchunguzi wa afya.(medical report)
  •  

MWISHO WA KUWASILISHA MAOMBI NI TAREHE 24/06/2019.



Share via Whatsapp

Others

Promoted Ads

No preview available
Highheels
623

Visits

TZS 25,000
No preview available
Dishdash
407

Visits

TZS 20,000
No preview available
Night dress
384

Visits

TZS 8,000
No preview available
saa za kike
436

Visits

TZS 15,000
No preview available
vyetezo vya umeme
392

Visits

TZS 10,000
No preview available
maua
326

Visits

TZS 7,000
No preview available
bulb
241

Visits

TZS 3,000

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili