Nafasi za Masomo Indonesia
General Description
Source: MOEZ
Release date: 2019-03-25
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar inatangaza nafasi za ufadhili wa masomo ya muda mrefu kwa ngazi ya shahada ya uzamili (Masters) kwa mwaka wa masomo 2019/2020
Kwa kufanya maombi, ingia katika tovuti:
KNB Scholarship 2019 – Indonesian Government Scholarship For Masters
Maombi yatumwe si zaidi ya tarehe 12, Aprili 2019.
Nakala ya fomu za maombi ziwasilishwe Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mazizini Zanzibar, katika Kitengo cha Uratibu wa Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia chumba namba 57.