Nafasi za Masomo Islamic Development Bank (IDB)
General Description
NAFASI ZA MASOMO ISLAMIC DEVELOPMENT BANK
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar inatangaza nafasi za ufadhili wa masomo ya shahada ya kwanza zinazotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kiislamu (IDB) kwa mwaka wa masomo 2017/18. Fani zinazotolewa ni:
1. Udaktari wa binadamu (Doctor of medicine)
2. Udaktari wa meno (Dentistry)
3. Ufamasia (Pharmacy)
4. Uhandisi (Engineering)
Waombaji wa nafasi hizo wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
1. Awe na umri usiozidi miaka 24 ifikapo Septemba 2017.
2. Awe na afya njema.
3. Awe na ufaulu mzuri wa daraja la kwanza au la pili wa masomo ya sayansi kwenye mitihani ya kidato cha sita.
4. Awe amemaliza katika skuli za sekondari za Zanzibar.
5. Awe Mzanzibari.
6. Awe tayari kuendelea na masomo katika vyuo vilivyopo nchini Malaysia au Uturuki.
Kila mwombaji anatakiwa awasilishe barua ya maombi kwa Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu na aambatishe nyaraka zifuatazo.
1. Fomu ya maombi ya nafasi za ufadhili wa masomo iliyojazwa kikamilifu.
2. Vivuli vya vyeti au matokeo ya mitihani (result slips) ya kidato cha nne na sita.
3. Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
4. Kivuli cha kitambulisho cha Mzanzibari.
5. Kivuli cha hati ya kusafiria (Passport)
Kwa maelezo zaidi na kupata fomu za maombi fungua kurasa zifuatazo:
IDB ANNOUNCEMENT
IDB SCHOLARSHIP BOND
IDB APPLICATION FORM
Barua na fomu za maombi ziwasilishwe katika ofisi za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu zilizopo Vuga kwa Unguja na Chakechake kwa Pemba.
Mwisho wa kuwasilisha maombi hayo ni tarehe 04 Agosti, 2017.
AHSANTENI.