Nafasi za Masomo Sudan
General Description
Source: MOEZ
Release date: 2019-04-13
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR INATANGAZA NAFASI ZA MASOMO ZILIZOTOLEWA NA MUNADHAMAT AL-DA’AWAH AL-ISLAMIA KWA NGAZI YA SHAHADA YA KWANZA KATIKA CHUO KIKUU CHA “INTERNATIONAL UNIVERSITY OF AFRICA KHARTOUM, SUDAN” KATIKA FANI MBALIMBALI ZIKIWEMO:
- Udaktari
- Uuguzi
- Ufamasia
- Uhandisi
- Uchumi
- Sheria
- Sharia na Lugha ya Kiarabu
- Uuguzi
Chuo kinatoa huduma ya chakula, malazi na masomo bure kwa wote watakao chaguliwa.
Fomu za maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 20,000/= tu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar chumba namba 57 zitaanza kutolewa tarehe 15/04/2019 hadi tarehe 20/04/2019.
SIFA ZA MUOMBAJI:
Awe amemaliza kidato cha sita au thanawi na kufaulu.
Muombaji lazima alete vyeti halisi (Original Academic Certificates)
KWA MAELEZO ZAIDI FIKA CHUMBA NAMBA 57 KITENGO CHA URATIBU WA ELIMU YA JUU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA MAZIZINI ZANZIBAR.