Nafasi za kazi Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Unguja na Pemba
General Description
Source: Utumishi Zanzibar
Release date: 2019-11-25
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-
1. Afisa Shughuli za Kiislamu Daraja la II “Nafasi 6” Unguja na “Nafasi 3” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Sheria na Shariah (Islamic Law) au Uchumi au Biashara yenye masomo ya Uchumi wa Kiislamu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe amefaulu masomo ya Dini na Kiarabu katika mtihani wa kidato cha nne.
• Awe na Uwezo wa kutumia Kompyuta
• Awe tayari kufanya kazi Wilayani.
Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.
• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.
Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 29 Novemba, 2019. wakati wa saa za kazi