Nafasi za kazi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar

General Description

Source: Utumishi Zanzibar



Release date: 2019-08-29



Duty Station: Zanzibar
17540 visits!... Deadline: 2019-09-04 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar kama ifuatavyo:-

1. Afisa Mipango Daraja la II “Nafasi 6” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Mipango au Uchumi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Afisa Ushirikiano wa Kimataifa Daraja la II “Nafasi 3” Unguja na “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uhusiano wa Kimataifa au Uhusiano wa Umma kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Afisa Kumbukumbu Daraja la II “Nafasi 1” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Utunzaji Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. Mpishi Mkuu Daraja la II “Nafasi 1” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Upishi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. Mpishi Msaidizi Daraja la III “Nafasi 1” Unguja 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Upishi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.


• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 04 Septemba , 2019 wakati wa saa za kazi.



Share via Whatsapp

Others

Promoted Ads

No preview available
Highheels
566

Visits

TZS 25,000
No preview available
Dishdash
365

Visits

TZS 20,000
No preview available
Night dress
343

Visits

TZS 8,000
No preview available
saa za kike
385

Visits

TZS 15,000
No preview available
vyetezo vya umeme
358

Visits

TZS 10,000
No preview available
maua
276

Visits

TZS 7,000
No preview available
bulb
203

Visits

TZS 3,000

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili