Nafasi za kazi ZSSF Zanzibar

General Description

Source: zssf website



Release date: 2020-06-24



Duty Station: Zanzibar
42698 visits!... Deadline: 2020-07-03 15:30:36

MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR

 

 Juni 22, 2020 

 

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI 

 

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa Sheria Na. 2 ya mwaka 1998, sheria ambayo ilifanyiwa marekebisho na kupelekea kuanzishwa upya kwa Sheria Na. 2 ya mwaka 2005. Madhumuni ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ni kuwarejeshea wanachama wake uwezo wa kifedha pale ambapo mwanachama hawezi kufanya kazi kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kustaafu kazi, maradhi na kufariki. 

 

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) unawatangazia vijana wenye sifa nafasi za kazi kwa ajili ya kujaza nafasi kwa afisi zake za Unguja na Pemba, kama ifuatavyo: 

 

1. Afisa Rasilimali Watu - Daraja la II 

 

“Nafasi 1” Unguja na “Nafasi 1” Pemba 

 

Sifa za Muombaji: 

• Awe ni Mzanzibari. 

• Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Rasilimali Watu au Utawala au Usimamizi wa Ajira "Labour Studies” au fani zinazolingana nazo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

• Awe na uwezo wa kutumia Kompyuta. 

• Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha.

 

2. Afisa Utawala - Daraja la II “Nafasi 1” Unguja 

 

Sifa za Muombaji: 

 

• Awe ni Mzanzibari. 

• Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Utawala wa Umma/Rasilimali watu au fani zinazolingana nazo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

• Awe na uwezo wa kutumia Kompyuta. 

• Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha. 

 

3. Afisa Miradi - Daraja la II “Nafasi 1” Unguja 

 

Sifa za Muombaji: 

• Awe ni Mzanzibari. 

• Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Mipango/Miradi/Uchumi au fani zinazolingana nazo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

• Awe na uwezo wa kutumia Kompyuta. 

• Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha. 

 

4. Afisa Masoko - Daraja la II “Nafasi 1” Unguja 

 

Sifa za Muombaji: 

 

• Awe ni Mzanzibari. 

• Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Masoko au fani zinazolingana nazo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

• Awe na uwezo wa kutumia Kompyuta. 

• Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha.

 

5. Mkaguzi wa ndani - Daraja la II “Nafasi 1” Unguja 

 

Sifa za Muombaji: 

 

• Awe ni Mzanzibari. 

• Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Uhasibu na Fedha pamoja na Teknolojia ya Habari au fani zinazolingana nazo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

• Awe na uwezo wa kutumia Kompyuta. 

• Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha. 

 

6. Afisa TEHAMA - Daraja la II “Nafasi 1” Unguja na “Nafasi 1” Pemba 

 

Sifa za Muombaji: 

 

• Awe ni Mzanzibari. 

• Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) au fani zinazolingana nazo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

• Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha. 

• Muombaji mwenye vyeti vya utaalamu (Professional Certificates) atapewa kipaombele. 

 

7. Afisa Ununuzi na Ugavi - Daraja la II “Nafasi 1” Unguja 

 

Sifa za Muombaji: 

• Awe ni Mzanzibari. 

• Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Manunuzi na Ugavi au fani zinazolingana nazo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

• Awe na uwezo wa kutumia Kompyuta. 

• Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha. 

• Muombaji mwenye uzoefu wa kazi za Manunuzi na Ugavi atapewa kipaombele. 

 

8. Afisa Ukaguzi na Ufatiliaji – Daraja la II “Nafasi 1” Pemba 

 

Sifa za Muombaji: 

• Awe ni Mzanzibari. 

• Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Uongozi wa Biashara au fani zinazolingana nazo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

• Awe na uwezo wa kutumia Kompyuta. 

• Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha. 

• Muombaji mwenye uzoefu wa kazi za Ukaguzi na Ufatiliaji atapewa kipaombele. 

 

9. Afisa muingizaji taarifa (Data entry officer) – Daraja la II “Nafasi 1” Unguja 

 

Sifa za Muombaji: 

• Awe ni Mzanzibari. 

• Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani “Record Management/Information Technology” au fani zinazolingana nazo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. • Awe na uwezo wa kutumia Kompyuta. 

• Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha. 

 

10. Mhandisi Umeme na mitambo - Daraja la II “Nafasi 1” Pemba 

 

Sifa za Muombaji: 

 

• Awe ni Mzanzibari. 

• Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya “Electric/Telecom Engineering” au fani zinazolingana nazo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

• Awe na uwezo wa kutumia Kompyuta. 

• Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha. 

• Muombaji mwenye uzoefu katika kazi za mitambo ya umeme atapewa kipaombele. 

 

11. Msaidizi Mhandisi Umeme - Daraja la II “Nafasi 1” Pemba 

 

Sifa za Muombaji: 

 

• Awe ni Mzanzibari. 

• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Umeme “Electric Engineering” au fani zinazolingana nazo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

• Awe na uwezo wa kutumia Kompyuta. 

• Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha. 

• Muombaji mwenye uzoefu katika kazi za mitambo ya umeme atapewa kipaombele. 

 

12. Dereva – Daraja la III “Nafasi 1” Pemba 

 

Sifa za Muombaji: 

 

• Awe ni Mzanzibari. 

• Awe amehitimu elimu ya Sekondari. 

• Awe na leseni halali ya Udereva Daraja la "C". 

• Awe na uzoefu wa kuendesha gari usiopungua miaka mitatu 

 

13. Tarishi Daraja la III “Nafasi 1” Unguja na “Nafasi 1” Pemba 

 

Sifa za Muombaji: 

 

• Awe ni Mzanzibari. 

• Awe amehitimu elimu ya Sekondari.

 

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE 

 

• Umri wa muombaji usizidi miaka 35. 

• Kwa upande wa Pemba, waombaji wanawake watapewa kipaumbele. 

• Watumishi walioko katika ajira za SMZ hawaruhusiwi kuomba. 

• Waombaji waliosoma vyuo vya nje ya nchi, wanatakiwa kuthibitisha vyeti vyao TCU 

 

BARUA ZA MAOMBI ZIAMBATANISHWE NA MAMBO YAFUATAYO: 

 

a) Kivuli cha Cheti cha Mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari). b) Vivuli vya Vyeti vya kumalizia masomo. 

c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa. 

d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari. 

e) Taarifa ya Wasifu binafsi (CV); tafadhali weka namba yako ya simu pamoja na namba za wadhamini 2 

f) Picha mbili (2) ya Passport Size zilizopigwa karibuni. 

 

N.B:

 

a) Vyeti vyote vilivyotajwa hapo juu lazima vithibitishwe na Mahakama. 

b) Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa. 

 

Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 3 Julai 2020 wakati wa saa za kazi.

 

 JINSI YA KUTUMA MAOMBI: 

 

Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar iliyopo Kilimani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Tawi la ZSSF, Tibirinzi Chake Chake Pemb Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo: 

 

MKURUGENZI MWENDESHAJI, 

MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR, 

S. L. P 2716 - ZANZIBAR



Share via Whatsapp

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili