Nafasi za kazi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati

General Description

Source: Utumishi Zanzibar



Release date: 2019-07-13



Duty Station: Zanzibar
10019 visits!... Deadline: 2019-07-19 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati kama ifuatavyo:-

1. Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utunzaji Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Katibu Muhtasi Daraja la III “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Uhazili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Taarishi Daraja la III “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari.

4. Msaidizi Afisa Takwimu Daraja la III “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Takwimu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. Karani Mahkama Daraja la III “Nafasi 1” 
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe na elimu ya Stashahada katika fani ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6. Walinzi Daraja la III “Nafasi 4”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Mafunzo ya Ulinzi kutoka JKU au JKT.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 19 Julai, 2019 wakati wa saa za kazi.



Share via Whatsapp

Others

Promoted Ads

No preview available
Highheels
538

Visits

TZS 25,000
No preview available
Dishdash
340

Visits

TZS 20,000
No preview available
Night dress
312

Visits

TZS 8,000
No preview available
saa za kike
364

Visits

TZS 15,000
No preview available
vyetezo vya umeme
334

Visits

TZS 10,000
No preview available
maua
250

Visits

TZS 7,000
No preview available
bulb
188

Visits

TZS 3,000

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili