Nafasi za kazi za Muda Makarani na Wasimamizi wa Sensa
General Description
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TANGAZO LA AJIRA ZA MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022
UTANGULIZI
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iko kwenye maandalizi ya kufanya Sensa ya Watu na Makazi ambayo itafanyika tarehe 23 Agosti 2022. Ili kufanikisha Sensa hii, Serikali inatangaza nafasi za kazi za muda za MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA kwa Watanzania wenye nia na sifa zinazostahili kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.
1. KARANI WA SENSA
a) Kazi za Kufanya
Mwombaji wa nafasi hii, endapo atachaguliwa atatakiwa kuhudhuria mafunzo ya makarani ambapo baada ya mafunzo ikiwa atafaulu atatakiwa kurejea katika eneo alilotokea au kupangiwa eneo lingine lolote kwa ajili ya kutekeleza kazi zifuatazo:-
- i) Kutambua mipaka ya eneo la kuhesabia watu kwa kulinganisha na ramani ya eneo la kuhesabia watu na maelezo ya mipaka yaliyopo kwenye ramani hiyo;
- ii) Kushirikiana na msimamizi na uongozi wa eneo husika kutambua kama katika eneo la kuhesabia watu kuna makundi maalaum yanayotakiwa kuhesabiwa kwa utaratibu maalum tofauti na kaya za kawaida;
- iii) Kuhoji dodoso la jamii katika ngazi ya kitongoji/mtaa/shehia;
- iv) Kuhesabu watu wote waliolala ndani ya mipaka ya eneo la kuhesabia watu usiku wa kuamkia siku ya Sensa ndani ya muda uliopangwa;