Nafasi za masomo (SMZ Scholarships) Bodi ya Mikopo Zanzibar
General Description
Nafasi za masomo (Scholarships) za Bodi ya mikopo Zanzibar
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar inatangaza nafasi kumi za ufadhili wa masomo kwa njia ya scholarship zinazotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa vijana waliofaulu vizuri zaidi mitihani yao ya kidato cha sita kwa mwaka 2017 na kufanikiwa kupata ufaulu wa daraja la kwanza katika masomo ya sayansi.
Masharti ya kuomba nafasi hizo ni:
- Muombaji awe ni Mzanzibari Mkaazi aliyehitimu kidato cha sita katika skuli za Sekondari za Zanzibar.
- Awe amefaulu vizuri masomo ya sayansi kwa kiwango cha daraja la kwanza.
- Atajiunga kusomea fani zinazohusiana na ufundi au Sayansi katika vyuo vya ndani vya Tanzania.
- Baada ya kuteuliwa mwanafunzi hatapaswa kuwa na mfadhili au mkopo mwengine wa kulipia masomo yake.
- Baada ya kuhitimu atapaswa kurudi nyumbani na kufanyakazi Zanzibar kwa kipindi kisichopungua miaka minne.
Watakaoteuliwa watalipiwa yafuatayo kwa kipindi chote cha
masomo ya shahada ya kwanza:
- Ada ya masomo na mitihani kwa 100%
- Gharama za chakula na malazi
- Gharama za vitabu
- Gharama za mafunzo ya vitendo
- Gharama za Vifaa vya kazi vya kujifunzia.
Fomu za maombi ya scholarship hizo zinapatikana katika ofisi za Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu zilizopo Vuga kwa Unguja na Chake Chake Pemba kuanzia tarehe 17/07/2017 hadi tarehe 15/08/2017
Maombi yatapaswa kuambatishwa na cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha Mzanzibari, matokeo ya mitihani kidato cha nne na sita, na picha ya muombaji.
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti za Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu Zanzibar (www.zhelb.go.tz) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
(www.moez.go.tz)
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15/08/2017.