Nafasi za masomo (Scholarships) Utabibu Mifugo China

General Description

Source: ZHELB



Release date: 2017-07-17


Download


Duty Station: CHina
8230 visits!... Deadline: 2017-08-15 00:00:00

Nafasi za masomo china Veterinary Medicine

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar inatangaza nafasi za masomo ya shahada ya kwanza ya Tiba ya Mifugo (Bachelor of Veterinary Medicine) katika Chuo Kikuu cha Yichun kilichopo katika jimbo la Jiangxi nchini China kwa mwaka wa masomo 2017/18. Masomo hayo yatatolewa kwa lugha ya Kichina.

 

Waombaji wa nafasi hizo wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

1.   Awe na umri usiozidi miaka 27 ifikapo Septemba 2017.

2.   Awe na afya njema.

3.   Awe na ufaulu mzuri wa masomo ya sayansi kwenye mitihani ya kidato cha sita au Diploma ya Kilimo au Diploma ya Mifugo.

4.   Awe Mzanzibari.

 

Kila mwombaji anatakiwa awasilishe barua ya maombi kwa Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu na aambatishe nyaraka zifuatazo:

1.   Vivuli vya vyeti au matokeo ya mitihani (result slips) ya kidato cha nne na sita au Diploma.

2.   Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.

3.   Kivuli cha kitambulisho cha Mzanzibari.

4.   Kivuli cha hati ya kusafiria.

 

Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar (www.zhelb.go.tz) na tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar (www.moez.go.tz).

Barua za maombi ziwasilishwe katika ofisi za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu zilizopo Vuga kwa Unguja na Chake Chake kwa Pemba.

Mwisho wa kuwasilisha maombi hayo ni tarehe 15 Agosti, 2017.

 

AHSANTENI.

 

 



Download

Share via Whatsapp

Others

Promoted Ads

No preview available
Highheels
623

Visits

TZS 25,000
No preview available
Dishdash
407

Visits

TZS 20,000
No preview available
Night dress
384

Visits

TZS 8,000
No preview available
saa za kike
436

Visits

TZS 15,000
No preview available
vyetezo vya umeme
392

Visits

TZS 10,000
No preview available
maua
326

Visits

TZS 7,000
No preview available
bulb
241

Visits

TZS 3,000

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili