Nafasi za masomo Oman Scholarships

General Description

Source: ZHELB



Release date: 2017-08-15


Download


Duty Station: Oman
7798 visits!... Deadline: 2017-08-18 00:00:00

NAFASI ZA MASOMO NCHINI OMAN MWAKA 2017/18

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar inatangaza nafasi za ufadhili wa masomo kwa njia ya scholarship zinazotolewa na Serikali ya Oman kwa vijana waliofaulu vizuri zaidi mitihani yao ya kidato cha sita kwa mwaka 2017 na kufanikiwa kupata ufaulu wa daraja la kwanza katika masomo ya sayansi na biashara.

Masharti ya kuomba nafasi hizo ni:

  • Ø Muombaji awe ni Mzanzibari
  • Ø Awe amehitimu kidato cha sita katika skuli za Sekondari za Zanzibar.
  • Ø Awe amefaulu vizuri masomo ya sayansi au biashara kwa kiwango cha daraja la kwanza.
  • Ø Awe tayari kusoma fani zinazohusiana na uhandisi, biashara au fedha katika vyuo vilivyopo Oman.
  • Ø Awe na umri usiozidi miaka 24 ifikapo Oktoba 2017.
  • Ø Awe amehitimu masomo ya kidato cha sita sio zaidi ya miaka miwili iliopita
  • Ø Awe na afya njema
  • Baada ya kuhitimu atapaswa kurudi nyumbani na kufanya kazi Zanzibar kwa kipindi kisichopungua miaka minne.

Fomu za maombi ya scholarship hizo zinapatikana katika tovuti za Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu Zanzibar (www.zhelb.go.tz) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali (www.moez.go.tz).

Fomu za maombi zinapaswa kuambatishwa na:

  1. Kivuli cha kitambulisho za Mzanzibari.

2. Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.

 

  1. Kivuli cha cheti cha kidato cha nne.
  2. Kivuli cha cheti/matokeo ya mitihani (result slip) ya kidato cha sita.
  3. Ithibati ya tabia njema (Certificate of good conduct) kutoka skuli aliyomalizia masomo.
  4. Taarifa ya uchunguzi wa afya (medical report).
  5. Picha sita za passport size.
  6. Kivuli cha hati ya kusafiria (Passport).

Mwisho wa kupokea maombi ni siku ya IJUMAA ya tarehe 18/08/2017 saa 9:30 mchana.

 

DOWNLOAD APPLICATION FORM KWENYE KIUNGANISHI HAPO JUU



Download

Share via Whatsapp

Others

Promoted Ads

No preview available
Highheels
623

Visits

TZS 25,000
No preview available
Dishdash
407

Visits

TZS 20,000
No preview available
Night dress
384

Visits

TZS 8,000
No preview available
saa za kike
436

Visits

TZS 15,000
No preview available
vyetezo vya umeme
392

Visits

TZS 10,000
No preview available
maua
326

Visits

TZS 7,000
No preview available
bulb
241

Visits

TZS 3,000

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili