Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Chuo cha UDSM na DUCE

General Description

Source: ajira.go.tz



Release date: 2023-01-23



Duty Station: TANZANIA
26716 visits!... Deadline: 2023-01-31 01:01:00

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

 

 Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es salaam (DUCE) anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 28 - 31 Januari, 2023 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo. 

 

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:- 

i. Usaili utafanyika 28 - 31 Januari, 2023 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada; 

ii. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask); 

iii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi; 

iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Leseniya Udereva, Kitambulisho cha Uraia, Barua ya utambulisho toka Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa/Kijiji unapoishi au Hati ya kusafiria; 

v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji; 2 

vi. Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI; 

vii. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi; 

viii. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili; 

ix. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA); 

x. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika; 

xi. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi; na 

xii. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.

 

KWA MAELEZO ZAIDI BONYEZA HAPA KWA KUONA MAJINA NA SEHEMU ZA USAILI



Share via Whatsapp

Others

Promoted Ads

No preview available
Highheels
631

Visits

TZS 25,000
No preview available
Dishdash
411

Visits

TZS 20,000
No preview available
Night dress
388

Visits

TZS 8,000
No preview available
saa za kike
444

Visits

TZS 15,000
No preview available
vyetezo vya umeme
397

Visits

TZS 10,000
No preview available
maua
328

Visits

TZS 7,000
No preview available
bulb
244

Visits

TZS 3,000

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili