Nafasi za Kazi ZFDA

General Description

Source: ZFDA website



Release date: 2020-10-25



Duty Station: Zanzibar
19172 visits!... Deadline: 2020-10-30 11:25:00

Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa chini ya  Sheria Namba 2/2006 na Marekebisho yake Namba 3/2017.

Lengo kuu la kuanzishwa Taasisi hii ni kusimamia Udhibiti wa Ubora na Usalama wa Chakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa vya Utibabu, ili kulinda Afya ya wazanzibar.

Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) inakaribisha maombi kwa ajili ya kujaza nafasi katika Ofisi yake ya Unguja na Pemba kwa waombaji wenye sifa stahiki.

 

Nafasi zenyewe ni:

1. MTAALAMU WA CHAKULA (FOOD SCIENTIST) DARAJA LA II

Nafasi mbili (2) Unguja na Nafasi mbili (2) Pemba
Sifa za Waombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Food Science and Technology kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
  • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

2. MFAMASIA (PHAMARCIST) DARAJA LA II

Nafasi tatu (3) Unguja

Sifa za Waombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe amehitimu Shahada ya Kwanza kwenye fani ya Famasia ‘Pharmacy’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
  • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
  • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada

3. DAKTARI WA WANYAMA (VETERINARY DOCTOR)  DARAJA LA II

Nafasi mbili (2) Unguja

Sifa za Muombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe amehitimu Shahada ya kwanza ya Udaktari wa Wanyama kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
  • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

4. AFISA MKAGUZI BIDHAA ZA MIFUGO DARAJA LA III

Nafasi saba  (7) Unguja  na mbili (2) Pemba

Sifa za Muombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe amehitimu Stashahada ya Animal health and production kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
  • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada

5. FUNDI SANIFU MADAWA (PHARMACEUTICAL TECHNICIAN) DARAJA LA III

Nafasi Tatu (3) Pemba

Sifa za Muombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe amehitimu Stashahada ya Famasia (Phamaceutical technician) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
  • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

6. AFISA TAKWIMU (STATISTICIAN) DARAJA LA II

Nafasi moja (1) Unguja.

Sifa za Muombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe na shahada ya kwanza ya Economics, Statistics au Commerce kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
  • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada

7. UCHUNGUZI WA VIMELEA (MICROBIOLOGIST) DARAJA LA II

Nafasi moja (1) Unguja.

Sifa za Muombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya “Microbiology” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
  • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

8. MUHANDISI  VIFAA VYA UTIBABU(BIOMEDICAL ENGINEER) DARAJA LA II

Nafasi mbili (2) Unguja.

Sifa za Muombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya “Biomedical Engineering” au “Biomedical Technology” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
  • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada

9. AFISA TEHAMA DARAJA LA II

Nafasi mbili (2) Unguja.

Sifa za Muombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Habari na Mawasiliano (ICT)’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
  • Awe na uzoefu wa kutumia na kusimamia mifumo ya kielektroniki
  • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada

10. MAINTENANCE AND CALIBRATION OFFICER (FUNDI VIFAA VYA MAABARA) DARAJA LA II

Nafasi moja (1) Unguja.

Sifa za Muombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe amehitimu Shahada ya Kwanza kwenye fani ya ‘Maintenance of Lab Equipment’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
  • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
  • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada

Jinsi ya Kuomba:

  • Muombaji anaweza kuwasilisha maombi yake moja kwa moja katika Ofisi ya Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi iliyopo Barabara ya Tomondo Mombasa Unguja wakati wa saa za kazi.
  • Kwa Waombaji walioko Pemba wanaweza kuwasilisha maombi yao katika Ofisi ya Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi iliopo Wete – Pemba.
  • Aidha muombaji anatakiwa aanishe nafasi ya kazi anayoiomba miongoni mwa zilizotajwa hapo juu.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-

  1. CV ya Muombaji.
  2. Kivuli cha cheti cha kumalizia masomo.
  3. Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari).
  4. Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
  5. Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
  6. Picha moja (1) ya Passport Size ilizopigwa karibuni.

ANGALIZO

Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ au kuomba nafasi zaidi ya moja maombi yake hayatazingatiwa.

Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 30 Oktoba, 2020, saa 9:30 Alaasiri.

Barua zote za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

MKURUGENZI MTENDAJI,
WAKALA WA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR

S.L.P 3595 – ZANZIBAR.



Share via Whatsapp

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili