Njia tano za kuomba nyongeza ya mshahara

General Description

Source: BBC SwahiliRelease date: 2023-01-31Duty Station: TANZANIA
13509 visits!... Deadline: 2023-12-31 05:45:00

Njia tano za kuomba nyongeza ya mshahara

 

Ikiwa unahisi kama mshahara wako uko chini ya inavyopaswa kuwa, labda hauko peke yako.

Katika maeneo kadhaa duniani, mishahara haijaongezeka licha ya kupanda kwa gharama za maisha.

Kuongeza mishahara ni hatua inayotarajiwa na wengi, hata zaidi katika muktadha huu. Ingawa hakuna uhakika kwamba mazungumzo na bosi wako yatasababisha ongezeko unalotaka, ingawa kuna njia za kuongeza nafasi za mafanikio.

Tulizungumza na waajiri, meneja na wanasaikolojia wa nchini Uingereza, ambao waliainisha vidokezo vitano kuhusu jinsi ya kujadili vyema nyongeza ya mishahara inayowezekana:

 

1. Chagua wakati unaofaa

Jill Cotton, mtaalamu wa mitindo anasema kuwa ni vyema kuandaa mazungumzo mapema kutakupa wewe na bosi wako muda wa kujiandaa na hivyo kufanya uwezekano mkubwa wa kujadili kwa tija.

"Usimshtukize bosi wako," anaeleza Cotton. "Mweleze kuwa unataka kufanya mazungumzo naye haswa kuhusu mshahara."

Rowsonara Begum, ambaye, pamoja na kaka yake, wanasimamia mgahawa wa Kihindi huko Uingereza, pia anaeleza kuwa kuna wakati mzuri wa kuzingatia hali ya biashara yenyewe: ikiwa mfanyakazi anawasilisha mahitaji yake katika kipindi ambacho biashara inafanya vizuri, kuna nafasi zaidi za mafanikio katika kuomba nyongeza ya mshahara.

 

2.Chukua ushahidi

Ikiwa unaomba nyongeza ya malipo, lazima uwe na hoja muhimu.

"Elewa unachofanya kazini, na umefanya nini ili kujiendeleza, kusaidia timu yako pamoja na wasimamizi wako ... Orodhesha faida zote za ulichofanya," anasema Shan Saba, mkurugenzi wa kampuni ya kuajiri ya Uingereza ya Brightwork. . .

Ushahidi huu wa kazi nzuri pia unamsaidia bosi wako kuelewa kwa nini unapaswa kulipwa zaidi, kulingana na Stephanie Davies, mwanasaikolojia ambaye ni mtaalamu wa maeneo ya kazi.

"Ubongo unahitaji 'kwanini': kwa nini nilipe kiasi hicho?", anatoa mfano.

Hata hivyo, sio tu kuhusu kubeba orodha ya mafanikio yako yote: Ni muhimu pia kuwa wazi kuhusu unachotaka kufanya baadaye, anasema Shan Saba.

"Ikiwa una matarajio ya kukua ndani ya shirika lako, kuwa na mpango wa nini unakusudia kufanya katika mwaka ujao.

 

3. Jiamini

Jill Cotton, kutoka Glassdoor, anasema kwamba mara nyingi watu hawajiamini na kuleta aina hii ya mada kwa sababu kuna "unyanyapaa" juu ya suala la malipo ambalo mtaalam anaamini kuwa ni "sehemu muhimu ya kazi".

 Wanawake na watu kutoka vikundi vya wachache wanaweza kupata ugumu wa kuomba nyongeza, anaongeza mwanasaikolojia Stephanie Davies.

 Anashauri ni vyema utafute aina fulani ya mshauri au mtu mwenye uzoefu ambaye anaweza kukusaidia kujitayarisha kwa mazungumzo haya. 

 

4. Ni vyema kujua kiasi cha nyongeza unayotaka akilini mwako

Wataalamu wengi wanakubali kwamba ni bora kuwa na kiasi kamili akilini kabla ya kuanza mazungumzo ya nyongeza.

Fanya utafiti wako, anashauri James Reed, rais wa kampuni ya kuajiri Reed.

 “Unaweza kupekua mtandaoni kwa ajili ya matangazo ya kazi na kuona mishahara ni ya kiasi gani kwa kazi zinazofanana,” anasema.

 Cotton anaonya kwamba kiasi lazima kiwe halisi.

"Sote tungependa kulipwa mamilioni kila mwaka.

 Lakini tunalipwa kufanya kazi kwa ujuzi tulionao," anasema.

 

5. Usikate tamaa

Ikiwa hatua zilizo hapo juu hazileti matokeo chanya ya nyongeza ya malipo, jaribu kutovunjika moyo.

"Wakati mwingine mazungumzo haya yanaweza kuchukua muda, hata miezi, lakini ni muhimu kuweka mawasiliano wazi," anasema Begum.

Mshahara sio kila kitu pia, anasema Reed.

"Siyo lazima tu kuhusu pesa. Unaweza kupata urahisi zaidi katika saa za kazi," anasema, akiongeza kuwa zana za ziada za mafunzo na maendeleo pia zinaweza kujadiliwa.

 Na ikiwa unahisi kama hupati kile unachotaka kutoka kwa mwajiri wako, kumbuka kwamba kuna fursa nyingine huko nje. 

"Unaweza kuangalia mahali pengine kila wakati, hiyo ndiyo zawadi kubwa," anasema Stephanie Davies.

 Share via Whatsapp

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili