Tangazo la Nafasi mbali mbali za Kazi Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA)

General Description

Source: ZAWARelease date: 2023-03-15Duty Station: Zanzibar
19965 visits!... Deadline: 2023-03-24 23:07:00

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

MAMLAKA YA MAJI ZANZIBAR INATANGAZA NAFASI ZA KAZI ZIFUATAZO: -

1. Afisa Takwimu Daraja la II (Pemba Nafasi 1)

Sifa za Msingi za Muombaji

a. Awe Mzanzibari.

b. Awe na Shahada ya kwanza katika fani ya Takwimu (Statistics), Uchumi (Economics), Mipango ya Kiuchumi (Economic Planning), au inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sifa za Ziada za Muombaji

a. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu ya kazi/nafasi anayoiomba

b. Awe ni mwenye stadi nyingi zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu sambamba na uwezo wa kukamilisha majukumu yake kwa wakati.

c. Awe na uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuzungumza Kiswahili na Kiingereza

2. Mhandisi Usambazaji Maji Daraja la II (Unguja Nafasi 2, Pemba Nafasi 1)

Sifa za Msingi za Muombaji:

a. Awe Mzanzibari.

b. Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani za Usambazaji Maji (Water Supply Engineering), Mazingira au inayolingana kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sifa za Ziada za Muombaji

a. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu ya kazi/nafasi anayoiomba.

b. Awe ni mwenye stadi nyingi zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu sambamba na uwezo wa kukamilisha majukumu yake kwa wakati.

c. Awe na uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuzungumza Kiswahili na Kiingereza

3. Mhandisi Rasilimali Maji Daraja la II (Unguja Nafasi 2, Pemba Nafasi 1)

Sifa za Msingi za Muombaji:

a. Awe Mzanzibari.

b. Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani za Usimamizi wa Rasilimali Maji {Water Resources Management), au inayolingana kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sifa za Ziada za Muombaji

a. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu ya kazi/nafasi anayoiomba.

b. Awe ni mwenye stadi nyingi zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu sambamba na uwezo wa kukamilisha majukumu yake kwa wakati.

c. Awe na uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuzungumza Kiswahili na Kiingereza

4. Mhandisi Makenika Daraja la II (Pemba Nafasi 1)

Sifa za Msingi za Muombaji:

a. Awe Mzanzibari.

b. Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani za Uhandisi Makenika ( Machenical Engineering) au inayolingana kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sifa za Ziada za Muombaji

a. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu ya kazi/nafasi anayoiomba.

b. Awe ni mwenye stadi nyingi zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu sambamba na uwezo wa kukamilisha majukumu yake kwa wakati.

c. Awe na uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuzungumza Kiswahili na Kiingereza

5. Mhandisi Ujenzi Daraja la II (Unguja Nafasi 2)

Sifa za Msingi za Muombaji

a. Awe ni Mzanzibari.

b. Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Uhandisi Ujenzi (Civil Engineering) au inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sifa za Ziada za Muombaji

a. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu ya kazi/nafasi anayoiomba.

b. Awe na uwezo wa kusanifu matangi ya maji, kusanifu mfumo wa mtandao wa maji na majengo.

c. Awe ni mwenye stadi nyingi zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu sambamba na uwezo wa kukamilisha majukumu yake kwa wakati.

d. Awe na uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuzungumza Kiswahili na Kiingereza.

6. Mhandisi Jiolojia Daraja La II (Unguja Nafasi 2, Pemba Nafasi 1)

Sifa za Msingi za Muombaji:

a. Awe ni Mzanzibari.

b. Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Jiolojia (Geologist), Hydrojiolojia (Hydrogeologist) au inayolingana kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sifa za Ziada za Muombaji

a. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu ya kazi/nafasi anayoiomba.

b. Awe na uwezo wa kupima na udongo.

c. Awe na uwezo wa kujua udongo sahihi katika pahali ambapo matenki ya maji yatajengwa.

d. Awe ni mwenye stadi nyingi zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu sambamba na uwezo wa kukamilisha majukumu yake kwa wakati.

e. Awe na uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuzungumza Kiswahili na Kiingereza.

7. Mhandisi Ukadiriaji Gharama za Ujenzi (Quantity Surveyor) Daraja La II (Unguja Nafasi 1)

Sifa za Msingi za Muombaji:

a. Awe ni Mzanzibari.

b. Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Uchumi wa Majengo (Building Economics) au inayolingana kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sifa za Ziada za Muombaji

a. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu ya kazi/nafasi anayoiomba.

b. Awe na uwezo wa kupitia na kutambua, na kuchora michoro/ramani maeneo.

c. Awe ni mwenye stadi nyingi zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu sambamba na uwezo wa kukamilisha majukumu yake kwa wakati.

d. Awe na uwezo mzuri wa kutumia kompyuta.

e. Awe na uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuzungumza Kiswahili na Kiingereza.

8. Afisa Usalama na Afya Kazini Daraja la II (Unguja Nafasi 1)

Sifa za Msingi za Muombaji:

a) Awe ni Mzanzibari

b) Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani za Usalama na Afya mahali pa kazi, au fani inayolingana kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sifa za Ziada za Muombaji

a. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu ya kazi/nafasi anayoiomba.

b. Awe na uwezo Kusimamia kikamilifu mambo yanayohusiana na usalama wa wafanyakazi na mali pahali pa kazi.

c. Awe ni mwenye stadi nyingi zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu sambamba na uwezo wa kukamilisha majukumu yake kwa wakati.

d. Awe na uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuzungumza Kiswahili na Kiingereza

9. Mchambuzi wa Kompyuta Daraja la II (Unguja Nafasi 1, Pemba Nfasi 1)

Sifa za Msingi za Muombaji:

a. Awe Mzanzibari.

b. Awe amehitimu Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Kompyuta au inayolingana kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sifa za Ziada za Muombaji

a. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu ya kazi/nafasi anayoiomba.

b. Awe na uwezo Kusimamia kikamilifu mambo yanayohusiana na Kompyuta, mifumo na mitandao.

c. Awe ni mwenye stadi nyingi zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu sambamba na uwezo wa kukamilisha majukumu yake kwa wakati.

d. Awe na uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuzungumza Kiswahili na Kiingereza.

10. Afisa Ufuatiliaji na Tathmini Daraja la II – (Unguja Nafasi 1, Pemba Nafasi 1)

Sifa za Msingi za Muombaji:

a. Awe ni Mzanzibari.

b. Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Ufuatiliaji na Tathmini (Monitoring & Evaluation) au inayolingana kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sifa za Ziada za Muombaji

a. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu ya kazi/nafasi anayoiomba.

b. Awe na uwezo wa kufuatilia, kupanga na kutathmini kazi za msingi za Taasisi.

c. Awe ni mwenye stadi nyingi zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu sambamba na uwezo wa kukamilisha majukumu yake kwa wakati.

d. Awe na uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuzungumza Kiswahili na Kiingereza

11. Afisa Usafirishaji Daraja La II (Unguja Nafasi 1)

Sifa za Msingi za Muombaji:

a. Awe ni Mzanzibari.

b. Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya fani ya Usafiri (Logistic & Transport) au inayolingana kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sifa za Ziada za Muombaji

a. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu ya kazi/nafasi anayoiomba.

b. Awe na uwezo wa kupanga na Kusimamia safari za kazi, kusimamia na kuvitunza vyombo vya usafiri vya Taasisi ikiwemo magari.

c. Awe ni mwenye stadi nyingi zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu sambamba na uwezo wa kukamilisha majukumu yake kwa wakati.

d. Awe na uwezo mzuri wa kutumia kompyuta.

e. Awe na uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuzungumza Kiswahili na Kiingereza.

12. Afisa Uhusiano Daraja la II (Pemba Nafasi 1)

Sifa za Msingi za Muombaji:

a. Awe Mzanzibari.

b. Awe amehitimu elimu ya shahada ya Kwanza ya Uhusiano wa Umma, Uhusiano wa Kimataifa, au fani inayolingana kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sifa za Ziada za Muombaji

a. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu ya kazi/nafasi anayoiomba.

b. Awe ni mwenye stadi nyingi zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu sambamba na uwezo wa kukamilisha majukumu yake kwa wakati.

c. Awe na uwezo wa kupokea na kusambaza taarifa kwa haraka iwe kwa njia za kawaida au za kielektroniki.

d. Awe na uwezo mzuri wa kuandika na kuwasilisha taarifa.

e. Awe na uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuzungumza Kiswahili na Kiingereza.

13. Afisa Sheria Daraja la II (Pemba Nafasi 1)

Sifa za Msingi za Muombaji

a. Awe Mzanzibari.

b. Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya Sheria au fani inayolingana kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sifa za Ziada za Muombaji

a. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu ya kazi/nafasi anayoiomba.

b. Awe na uwezo wa kuchambua na kusimamia sheria, mikataba, mali za Taasisi na haki katika misingi ya kisheria.

c. Awe ni mwenye stadi nyingi zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu sambamba na uwezo wa kukamilisha majukumu yake kwa wakati.

d. Awe na uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuzungumza Kiswahili na Kiingereza

14. Fundi Mchundo Magari Daraja la III (Unguja Nafasi 1)

Sifa za Msingi za Muombaji:

a. Awe Mzanzibari.

b. Awe amehitimu Ngazi ya Stashahada ya Kawaida katika fani ya Ufundi Makenika au inayolingana kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sifa za Ziada za Muombaji

a. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu ya kazi/nafasi anayoiomba.

b. Awe ni mwenye stadi nyingi zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu sambamba na uwezo wa kukamilisha majukumu yake kwa wakati.

c. Awe na uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuzungumza Kiswahili na Kiingereza

15. Fundi Mchundo Maji Daraja la III (Unguja Nafasi 2, Pemba nafasi 1)

Sifa za Msingi za Muombaji:

a. Awe Mzanzibari.

b. Awe amehitimu Ngazi ya Stashahada ya Kawaida katika fani ya Ufundi Bomba, Usambazaji Maji, Mekatroniki, Rasilimali Maji, au inayolingana kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sifa za Ziada za Muombaji

a. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu ya kazi/nafasi anayoiomba.

b. Awe ni mwenye stadi nyingi zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu sambamba na uwezo wa kukamilisha majukumu yake kwa wakati.

c. Awe na uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuzungumza Kiswahili na Kiingereza

16. Afisa Msaidizi Biashara Daraja La III (Pemba Nafasi 1)

Sifa za Msingi za Muombaji

a. Awe ni Mzanzibari.

b. Awe amehitimu Ngazi ya Stashahada ya Kawaida katika fani za Biashara, Masoko au inayolingana kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Sifa za ziada za Muombaji

a. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu ya kazi/nafasi anayoiomba.

b. Awe ni mwenye stadi nyingi zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu sambamba na uwezo wa kukamilisha majukumu yake kwa wakati.

c. Awe na uwezo mzuri wa kusoma, kuandika na kuzungumza Kiswahili na Kiingereza.

JINSI YA KUOMBA

Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

MKURUGENZI MKUU,

MAMLAKA YA MAJI ZANZIBAR,

P.O. BOX 460,

ZANZIBAR.

Au awasilishe ombi lake moja kwa moja katika Afisi Kuu za Mamlaka ya Maji Zanzibar- Msikiti Mabluu.

Kwa waombaji wa nafasi za Pemba wawasilishe maombi yao moja kwa moja Afisi Kuu za Mamlaka ya Maji Pemba- Chakechake.

Kila muombaji anatakiwa kuainisha nafasi ya kazi anayoiomba, vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

BARUA ZA MAOMBI ZIAMBATANISHWE NA VIELELEZO VIFUATAVYO: -

a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo kwa mujibu wa Kada husika.

b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari “A” level/” O” level).

c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.

d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.

e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.

TANBIHI:

a) Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progress Report’ maombi yake hayatazingatiwa.

b) Muombaji anatakiwa azingatie masharti yaliyomo katika Tangazo hili.

c) Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 24/03/2023 wakati wa kumalizika saa za kazi (saa 9:30 jioni).Share via Whatsapp

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2023 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili