Mhandisi Umeme (Electrical Engineer) Daraja la II-UNGUJA - 1 POST
EMPLOYER
OFISI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI (CAG)
APPLICATION TIMELINE:
From: 27-03-2024 To: 12-04-2024
DUTIES AND RESPONSIBILITIES
Kukagua mifumo ya umeme na kufanya matengenezo madogo madogo katika majengo ya Serikali
Kufanya ukaguzi wa usanifu wa miradi mbali mbali ya umeme
Kukagua na kusimamia hali ya ufungaji mashine katika taasisi za Srikali
Kufanya kazi ya kutengeneza mitambo na mifumo ya umeme ya Ofisi
Kufanya Ukaguzi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali ikiwemo na miradi mbalimbali ya umeme
Kusaidia katika kutambua maeneo yanayoweza kufanyiwa Ukaguzi pamoja na kutunza na kuhifadhi taarifa mbalimbali juu ya Ukaguzi
Kusaidia katika uandaaji wa mipango kazi ya Ukaguzi
Kusaidia katika kuandaa ripoti ya utafiti wa awali pamoja na Mipango ya Kazi itakayosaidia katika kufanya Ukaguzi
Kukusanya taarifa na nyaraka za ukaguzi kwa ajili ya kufanya Ukaguzi
Kusaidia katika kuchakata taarifa na kuandaa ripoti za Ukaguzi
Kusaidia katika kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo ya Kaguzi zilizokwishafanyika
Kusaidia katika uandaaji wa taarifa za ufuatiliaji wa mapendekezo ya Ukaguzi
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi zinazoendana na sifa na fani yake.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uhandisi Umeme kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na awe amesajiliwa na Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB).
Awe na umri usiozidi miaka 46
Barua za maombi ziwasilishwe na mambo yafuatayo:-
Maelezo binafsi ya muombaji (CV).
Vivuli vya vyeti vya kumalizia masomo na kwa aliyesoma nje ya Tanzania anatakiwa kuambatanisha kivuli cha cheti cha uthibitisho kutoka TCU.
Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
Kivuli cha kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.
Picha ya rangi ya muombaji ya karibuni (Current Colored Passport Size Picture).