Nafasi za Kazi Shirika la Biashara la Taifa ZSTC

General Description

Source: ZSTC Website



Release date: 2018-03-08


Download


Duty Station: Zanzibar
29133 visits!... Deadline: 2018-04-09 15:30:00

SHIRIKA LA BIASHARA LA TAIFA (ZSTC)

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) lilianzishwa mwaka 1968 chini ya Sheria Na. 1 ya mwaka 1966 Sheria ya Mashirika ya Umma, kupitia tamko la Kisheria (Legal Notice) Na. 39 ya mwaka 1968.

Shirika limepewa jukumu la kusimamia maendeleo ya sekta ya karafuu Zanzibar, pamoja na mazao mengine ya biashara, kuzalisha mafuta ya mimea na kusimamia shughuli zote zinazohusiana na usambazaji wa mazao ya Biashara ya Taifa.

Shirika la ZSTC, kwa sasa linafanya shughuli zake chini ya Sheria ya Shirika la Biashara la Taifa Na. 11 ya mwaka 2011.

Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) linatangaza nafasi zakazi kama ifuatavyo :-

  1. AFISA MIPANGO – UNGUJA NAFASI (2) Majukumu ya kazi.
    1. Kutayarisha mapendekezo ya sera na mipango ya miradi katika Sekta mbali mbali.
    2. Kutoa ushauri wa maeneo ya kuelekeza utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
  • Kubuni miradi ya maendeleo katika maeneo/sekta inayohitajika.
  1. Kufanya uchambuzi wa kiutendaji wa miradi iliyopo kwenye

Shirika.

  1. Kuratibu makisio ya mapato na matumizi.
  2. Kufuatilia fedha za matumizi ya uendeshaji wa miradi kama ilivyokubaliwa katika bajeti.
  • Kuainisha na kuchambua matokeo ya taarifa za ufuatiliaji na tathmini.
  • Kutoa ushauri wa kitaalam na mapendekezo kwa miradi husika. ix. Kutayarisha ripoti ya ufuatiliaji na tathmini kwa kota.
  1. Kushiriki katika program ya mipango na bajeti ya Shirika.
  2. Kuhakikisha kwamba mipango ya tathmini na ufuatiliaji inatekelezwa ipasavyo.
  • Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yako kama atakavyopangiwa na Mkuu wako.

Sifa za Muombaji .

  1. Awe ni Mzanzibari.
  2. Awe na Elimu ya Shahada ya kwanza katika fani ya “Economy & Planning” kutoka katika Chuo kinachotambulika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  3. Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
  1. AFISA MANUNUZI NA UGAVI – NAFASI (2).

UNGUJA NAFASI (1) NA PEMBA NAFASI (1).

Majukumu ya kazi.

  1. Kuratibu shughuli zote za manunuzi ya bidhaa za Shirika Kuhakikisha kuwa manunuzi ya bidhaa yanafanyiwa maandalizi ya kutosha ili kufanikisha utekelezaji wake.

iii. Kufanya manunuzi ya bidhaa zote za Shirika na kuhakikisha kuwa mahitaji mbali mbali yanapatikana. iv. Kuhakikisha kwamba idadi ya bidhaa zote zinazonunuliwa zinalingana na idadi iliyokabidhiwa ghalani.

  1. Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yako kama atakavyopangiwa na Mkuu wako. Sifa za Muombaji.
    1. Awe ni Mzanzibari.
    2. Awe na Elimu ya Shahada ya kwanza katika fani ya “Procurement & Supply Management” kutoka katika Chuo kinachotambulika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
    3. Awe na ujuzi wa Kompyuta.
  1. MSAIDIZI MAABARA KIWANDA CHA MAKONYO PEMBA –NAFASI 1

 Majukumu ya kazi.

  1. Kufanya uchunguzi wa mafuta ya miti mbali mbali.
  2. Kufanya uchungazi wa vitu mbali mbali vinavyotokana na mafuta.
  • Kufanya kazi nyengine utakazopangiwa na Mkuu wako wa kazi.

Sifa za Muombaji.

  1. Awe ni Mzanzibari.
  2. Awe na Elimu ya Shahada ya kwanza katika fani ya “Chemistry” kutoka katika Chuo kinachotambulika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  3. Awe na ujuzi wa Kompyuta.
  1. MHANDISI MITAMBO KIWANDA CHA MAKONYO PEMBA-NAFASI 1

Majukumu ya kazi 

  1. Mtendaji na msimamizi wa shughuli zote za ufundi kiwandani.
  2. Kumshauri Mkurugenzi wa Kiwanda katika shughuli za ufundi. ii. Kufanya kazi nyengine utakazopewa na Mkuu wako wa kazi.

Sifa za Muombaji.

  1. Awe ni Mzanzibari.
  2. Awe na Elimu ya Shahada ya kwanza katika fani ya “Mechanical Engineering” kutoka katika Chuo kinachotambulika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  3. Awe na ujuzi wa Kompyuta.
  1. MSIMAMIZI UZALISHAJI (PRODUCTION FOREMAN)

KIWANDA CHA MAKONYO – PEMBA NAFASI (1)

Majukumu ya kazi 

  1. Kupanga ratiba ya uzalishaji na kuhakikisha kuwa malengo ya uzalishaji yanafikiwa.
  2. Kutoa na kudhibiti utowaji wa vibali vya kutolea mali ghafi ghalani.
  • Kusimamia kazi nyengine kama matatizo ya viwango kadri inavyo gunduliwa na maabara.
  1. Kusimamia urekebishaji wa Paramita kama vile Temperature, Prussure, na Flurrates kutokana na aina ya mafuta yanayo zalishwa.
  2. Kuhakikisha kuwa purification unit zinafanya kazi ipasavyo katika hali ya usafi.
  3. Kuripoti kwa Mkuu wako wa Idara ya Ufundi matengenezo yote yanayohitajika.

Sifa za Muombaji.

  1. Awe ni Mzanzibari.
  2. Awe na Elimu ya Shahada ya kwanza katika fani ya “Chemical Engineering” au Machanical Engineering” kutoka katika Chuo kinachotambulika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  3. Awe na ujuzi wa Kompyuta.

JINSI YA KUTUMA MAOMBI:

Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake kwa njia ya Posta au moja kwa moja Makao Makuu ya Shirika yaliyopo Maisara Zanzibar wakati wa saa za kazi.

Barua za maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo :-

  1. Maelezo binafsi ya muombaji (CV).
  2. Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo.
  3. Kivuli cha Cheti cha Mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari).
  4. Kivuli cha Cheti cha kuzaliwa.
  5. Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari
  6. Picha moja (1) ya “Passport Size” iliyopigwa karibuni.

Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 09 April, 2018 wakati wa saa za kazi.

Barua za maombi ziandikwe kwa mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo :-

MKURUGENZI MWENDESHAJI

SHIRIKA LA BIASHARA LA TAIFA ZANZIBAR (ZSTC)

S.L.P. 26

ZANZIBAR.

Muombaji anatakiwa ainishe nafasi ya kazi anayoiomba kati ya zilizotajwa hapo juu vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Browse Ruwix, the portal dedicated to puzzle programs and tutorials.



Download

Share via Whatsapp

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili