Nafasi za Kazi Zanzibar Bureau of Standards (ZBS)

General Description

Source: ZBS web



Release date: 2018-04-16



Duty Station: Zanzibar
13576 visits!... Deadline: 2018-04-25 15:30:00

 

TAASISI YA VIWANGO YA ZANZIBAR (ZBS)  

 

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI 

 

Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Viwango ya Zanzibar Na.1 ya 2011. 

 

Lengo kuu la kuanzishwa Taasisi ya Viwango ya Zanzibar ni kuhakikisha kuwa Zanzibar inakua na viwango kwa ajili ya bidhaa na huduma na kusimamia ubora wa bidhaa na huduma hizo.   Viwango  na bidhaa  zenye  ubora zinalenga kulinda afya na usalama wa watumiaji pamoja na kukuza uchumi wa Zanzibar na kuhifadhi  mazingira ya nchi. 

 

Taasisi ya Viwango ya Zanzibar (ZBS) inakaribisha maombi ya kujaza nafasi tupu katika kada mbali mbali kwa waombaji wenye sifa stahili katika Ofisi yake iliyopo Unguja na Pemba. 

 

Nafasi zenyewe ni kama zifuatazo:- 

 

UNGUJA 

 

1. AFISA UKAGUZI  NA UDHIBITI UBORA DARAJA LA II – Nafasi mbili 

 

 Sifa za muombaji: 

 

•        Awe ni Mzanzibari

 

•        Awe na Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu au Stashahada ya uzamili ya sayansi ya kompyuta au fani inayolingana kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

 

•        Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta. 

 

•        Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.  

 

2.    AFISA UKAGUZI NA UDHIBITI UBORA MSAIDIZI DARAJA LA III – Nafasi mbili 

 

     Sifa za muombaji: 

 

•        Awe ni Mzanzibari. 

 

•        Awe na Stashahada ya kawaida (Ordinary Diploma) ya umeme, elektroniki au fani inayolingana kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

 

•        Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta. 

 

 

 

•        Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

 

 

 

 

 

 

 

2.    AFISA MAABARA UMEME DARAJA LA II – Nafasi moja

 

 

 

 

 

 

 

     Sifa za muombaji:

 

 

 

•        Awe ni Mzanzibari.

 

 

 

•        Awe na Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu au Stashahada ya uzamili ya umeme na elektroniki au fani inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 

 

 

•        Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

 

 

 

•        Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

 

 

 

 

 

 

 

3.    AFISA MAABARA UHANDISI MITAMBO DARAJA LA II – Nafasi moja

 

 

 

 

 

 

 

     Sifa za muombaji:

 

 

 

 

 

 

 

•        Awe ni Mzanzibari.

 

 

 

•        Awe na Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu au Stashahada ya uzamili ya uhandisi mitambo au fani inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

•        Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta. 

•        Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.  

4.    AFISA MAABARA UHANDISI MAJENGO DARAJA LA II – Nafasi moja  

    Sifa za muombaji: 

•        Awe ni Mzanzibari. 

•        Awe na Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu au Stashahada ya uzamili ya uhandisi majengo au fani inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

•        Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta. 

•        Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada. 

5.    AFISA VIWANGO DARAJA LA II – Nafasi tatu 

     Sifa za muombaji: 

•        Awe ni Mzanzibari. 

•        Awe na Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu au Stashahada ya Uzamili ya Sayansi ya biolojia, kemia, chakula, mazingira au fani inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

•        Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta. 

 

•        Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada. 

 

6.    AFISA UTHIBITI UBORA DARAJA LA II - Nafasi moja      Sifa za muombaji: 

 

•        Awe ni Mzanzibari. 

 

•        Awe na Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu au Stashahada ya Uzamili ya sayansi ya biolojia, chakula au fani inayolingana kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

 

•        Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta. 

 

•        Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.  

 

 

 

7.    AFISA MCHAMBUZI WA MIFUMO YA KOMPYUTA/AFISA WA MIFUMO YA KOMPYUTA/ AFISA WA MITANDAO YA KOMPYUTA/ AFISA WA DATABEZI 

 

DARAJA LA II – Nafasi tatu 

 

 

 

     Sifa za muombaji: 

 

•        Awe ni Mzanzibari. 

 

•        Awe na Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu au Stashahada ya Uzamili katika fani ya sayansi ya kompyuta au fani inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

 

•        Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada. 

 

8.    DEREVA DARAJA LA III - Nafasi mbili      

 

 

 

     Sifa za muombaji: 

 

•        Awe ni Mzanzibari. 

 

•        Awe na cheti cha Kidato cha nne (F.IV) na kupata leseni ya udereva wa gari kutoka Taasisi inayotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

 

 

 

    OFISI KUU PEMBA 

 

2.    AFISA UKAGUZI NA UDHIBITI UBORA DARAJA LA II – Nafasi mbili 

 

     Sifa za muombaji: 

 

•        Awe ni Mzanzibari

 

•        Awe na Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu au Stashahada ya uzamili ya sayansi ya biolojia, kemia, chakula au fani inayolingana kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

•        Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta. 

•        Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada. 

NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI 

Muombaji anatakiwa aandike barua ya maombi na kuambatanisha na barua hiyo: 

a)   Vivuli vya vyeti vya kumalizia masomo.   

b)   Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa. 

c)   Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari. 

d)   Picha moja ya Muombaji (Passport size). 

e)   Majina na anuani za Wadhamini wawili wanaotambulika. 

f)     Anuani rasmi anayopatikana muombaji, barua pepe na nambari ya simu. 

MAMBO YA KUZINGATIWA 

i.          Muombaji atakaewasilisha “Statement of Result” au “Progressive Report” maombi yake hayatazingatiwa. 

ii.         Muombaji anatakiwa aainishe nafasi moja anayoiomba kati ya zilizotajwa hapo juu vinginevyo maombi yake hayatazingatiwa.   

iii.        Asiwe muajiriwa wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

iv.       Barua   za maombi ziandikwe kwa mkono na ziwasilishwe moja kwa moja Ofisi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar iliyopo Eneo la Viwanda Amani wakati wa saa za kazi. 

v.        Kwa nafasi za uajiri kwa Ofisi ya ZBS Pemba waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi yao katika Ofisi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar iliyopo Chake Chake Pemba jirani na Benki ya NMB. 

vi.       Siku ya mwisho ya kupokea maombi ni Ijumaa tarehe 20 Aprili, 2018 saa 

9.30 alaasiri. vii. Mawasiliano   yatafanywa  kwa  wale  tu  watakaopita  katika  mchujo wa awali (short  listed). 

Maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo:- 

MKURUGENZI MKUU, 

TAASISI YA VIWANGO ZANZIBAR, 

S.L.P 1136, 

ZANZIBAR.  

Tangazo  hili  linapatikana pia  katika  Tovuti  ya  Taasisi  ya  Viwango  Zanzibar (ZBS) ambayo  ni  www.zbs.go.tz.

  



Share via Whatsapp

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili