Nafasi za kazi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ

General Description

Source: Utumishi Zanzibar



Release date: 2018-04-29



Duty Station: Zanzibar
11543 visits!... Deadline: 2018-05-04 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Pemba kama ifuatavyo:-

MKUU WA MKOA WA KUSINI - PEMBA:

1.Mlinzi Daraja la III “Nafasi 2” Pemba

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata mafunzo ya Ulinzi kutoka JKU au JKT.

2.Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 1” Pemba

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

WILAYA YA CHAKE CHAKE - PEMBA:

3.Afisa Ustawi Daraja la II “Nafasi 1” - Pemba 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Ustawi wa Jamii kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

4.Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 1” Pemba

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5.Mlinzi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata mafunzo ya Ulinzi kutoka JKU au JKT.

WILAYA YA MKOANI - PEMBA:

6.Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 2” Pemba

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

7.Mwangalizi wa Ofisi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utawala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

8.Mlinzi Daraja la III “Nafasi 1” Pemba

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata mafunzo ya Ulinzi kutoka JKU au JKT.

Jinsi ya Kuomba:

•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 04 Mei, 2018 wakati wa saa za kazi.



Share via Whatsapp

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili