Nafasi za Kazi Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto

General Description

Source: Utumishi Zanzibar



Release date: 2019-03-29



Duty Station: Zanzibar
14531 visits!... Deadline: 2019-04-05 15:30:00

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto kama ifuatavyo:-



1.Afisa Vyama vya Ushirika Daraja la III “Nafasi 5” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu ya Shahada ya Kwanzakatika fani ya Biashara au Uhasibu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar


2.Afisa Takwimu Daraja la III “Nafasi 1” 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu ya Stashahada katika fani ya Takwimu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

3.Mhudumu Daraja la III “Nafasi 2 

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari 

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 05 Aprili, 2019 wakati wa saa za kazi.



Share via Whatsapp

+ Tafadhali weka maoni yako hapa..

Advertise with us

© 2024 Zenji Shoppazz . All rights reserved | Design by W3layouts and Zenji Shoppazz Choose language : Kiswahili