Maelezo ya Bidhaa
UJUE UGONJWA WA PID (PELVIC INFRAMMATORY DISEASE)
Bei
Maelewano
Maelezo kiufupi :
UJUE UGONJWA WA PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE).
MAANA YA PID??????
__________________________________________
Pelvic Infalammatory Disease (PID) ni maambukizi kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke. PID hutokea pale bakteria waenezwao kwa ngono wanaposambaa kutoka kwenye uke (vagina) hadi....
Hali (Mpya/imetumika?):
Mpya
Inapatikana wapi:
Dar es salaam, Ilala boma
Jina la duka/Muuzaji:
Liwaya herbal
Mawasiliano:
Maelezo Zaidi
UJUE UGONJWA WA PID (PELVIC INFRAMMATORY DISEASE)
UJUE UGONJWA WA PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE). MAANA YA PID?????? __________________________________________ Pelvic Infalammatory Disease (PID) ni maambukizi kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke. PID hutokea pale bakteria waenezwao kwa ngono wanaposambaa kutoka kwenye uke (vagina) hadi kwenye nyumba ya uzazi (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na ovari. Dalili za PID huweza kuwa ni ngumu kueleweka. Baadhi ya wanawake hawaoni dalili zo zote. Kwa maana hiyo, unaweza usihisi cho chote hadi pale utakaposhindwa kupata ujauzito au hadi utakapoanza kupata maumivu ya kiuno. DALILI ZA PID ___________________ PID inaweza isilete dalili zo zote mbaya na ndogo zikitokea zinaweza kuwa ngumu kuzigundua. Baadhi ya wanawake hawapati dalili zo zote. Pale zinapojitokeza, zinaweza kuwa: ?? Maumivu – yanaweza kuwa madogo au makali – maeneo ya chini ya tumbo au nyonga ?? Uchafu usio wa kawaida au mzito ambao unaweza kuwa na harufu mbaya ?? Kutokwa damu kusiko kwa kawaida, hasa wakati wa tendo la ndoa, au katikati ya siku ?? Maumivu wakati wa kujamiiana ?? Homa, wakati mwingine kusikia baridi ?? Maumivu wakati wa haja ndogo, haja ndogo ya mara kwa mara au haja ndogo kutoka kwa shida. CHANZO CHA PID ___________________________________________ Kuna bakteria wa aina nyingi wanaoweza kusababisha PID, lakini maambukizi ya gonorrhea na chlamydia ndiyo yanayoonekana zaidi. Bakteria hao huambukiza wakati tendo la ndoa linapofanyika bila ya kutumia kinga. NJIA YA KUSAMBAA KWA PID ________________________________ Aghalabu, bakteria hawa huingia kwenye viungo ya uzazi vya mwanamke pale ulinzi wa kwenye shingo ya kizazi (cervix) unapovurugwa. Hii inaweza kutokea mathalani, wakati wa hedhi na baada ya kuzaa, mimba kuharibika au kutoa mimba. Mara chache bakteria huweza kujipenyeza wakati kifaa cho chote cha tiba kinapoingizwa kwenye nyumba ya uzazi. MAZINGIRA HATARISHI YA KUPATA PID ________________________________________________ Kuna vipengele ambavyo huweza kukuweka kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata PID, navyo ni: . Kuwa mwanamke uliye chini ya miaka 25 unayeshiriki ngono . Kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja . Kuwa na mahusiano na mpenzi mwenye wapenzi zaidi ya mmoja . Kufanya mapenzi bila kinga . Kujisafisha na maji mara kwa mara . Kuwa uliwahi kupata PID kabla au magonjwa mengine ya ngono MADHARA YATOKANAYO NA PID ___________________________________________ PID ambayo haikupata tiba inaweza kusababisha makovu na vifuko vyenye maji yenye wadudu kwenye mkondo wa njia ya uzazi ya mwanamke. Vitu hivi vinaweza kusababisha madhara ya kudumu kwenye viungo vya uzazi. Madhara yanayoweza kutokea ni pamoja na: ?? Mimba nje ya mirija (ectopic pregnancy). PID ndiyo sababu kubwa ya mimba kutunga nje ya kizazi. Mimba huweza kutunga nje ya kizazi endapo PID imesababisha makovu ndani ya mirija ya uzazi. Makovu haya husababisha yai lililopevushwa kushindwa kusafiri ndani ya mirija ya uzazi kuelekea kwenye nyumba ya uzazi. Badala yake yai hunata ndani ya mirija ya uzazi . Mimba nje ya kizazi husababisha utokaji wa damu usio wa kawaida unaoweza kukatisha maisha ya mwanamke. ?? Ugumba. Uharibifu wa viungo vya uzazi huweza kusababisha ugumba – kushindwa kupata ujauzito. Kadiri unavyozidi kupata PID mara nyingi zaidi, ndivyo hatari ya ugumba inavyozidi. Kuchelewa kupata tiba ya PID kunaongeza hatari ya ugumba. ?? Maumivu sugu ya nyonga. PID inaweza kusababisha maumivu ya nyonga yanayoweza kudumu kwa miaka mingi. Makovu ndani ya mirija ya uzazi na viungo vingine vya uzazi huweza kuleta maumivu wakati wa kujamiiana na wakati yai linadodondoshwa (ovulation). ?? Tubo-ovarian abscess. PID huweza kusababisha kutunga kwa usaha na kufanya majipu ndani ya njia ya uzazi. Mara nyingi majibu haya hutokea ndani ya mirija ya uzazi na ovari, ingawa huweza kuota ndani ya nyumba ya uzazi na shingo ya kizazi. Kama tiba haitatolewa, unaweza kupata maambukizi hatarishi kwa maisha. Tiba Ya PID Tiba ya mara moja kwa kutumia dawa itaondoa maambukizi yaliyosababisha PID. Lakini, hakuna njia ya kukarabati makovu au uharibifu kwenye njia ya viungo vya uzazi uliotokana na PID. Tiba ya PID yaweza kuwa: ?? Antibiotics. Daktari atakuandikia dawa inayoendana na chanzo cha tatizo lako. Utasubiri siku kama tatu kuona kama dawa ulizopewa zinafanya kazi. ?? Kumtibu Mwezi wako. Kuzuia maambukizi, yafaa mwezi wako afanyiwe uchunguzi na atibiwe. - Kuacha kushiriki ngono kwa muda. Acha kushiriki ngono hadi utakapomaliza tiba na kuona kuwa umepona. U R O G E T I X 5 ____________________ Ni dawa asilia yenye uwezo mkubwa wa kutibu maambukizi katika njia ya mkojo na maambukizi katika via vya Uzazi.Dawa hii ni tiba ya Uhakika na ya haraka kwa matatizo yafuatayo:???????? ?? Maambukizi katika via vya Uzazi (Pelvic inflammatory disease)-- *PID* ?? Kutokwa na Uchafu sehemu ya siri ya Mwanamke-- *Vaginal discharge.* ?? Kisonono-- *Ghonorrhea* ?? Kaswende-- *Syphilis* ?? Maambukizi katika njia ya Mkojo (Urinary Track Infections)-- *UTI* Dr Liwaya Tiba Asilia Tanzania +255755162724 +255717541527 muhammadliwaya@gmail.com
Mtandao huu una bidhaa nzuri tena zenye bei nafuu, Kila ninapotafuta bidhaa kwanza huja hapa na huweza kujipatia mahitaji yangu kwa bei poa, Naipendekeza kwa yeyote anayetafuta bidhaa bora. Hongera kwa waendeshaji wa website hii..
- Vitu vyenye ubora wa hali ya juu
- Bidhaa Oriji
- Bei zenye kununulika
- Huduma kwa wateja nzuri
- Mahali pamoja kwa mahitaji yote
- Gerentii
- Mitindo ya kisasa
Mtandao huu una bidhaa nzuri tena zenye bei nafuu, Kila ninapotafuta bidhaa kwanza huja hapa na huweza kujipatia mahitaji yangu kwa bei poa, Naipendekeza kwa yeyote anayetafuta bidhaa bora. Hongera kwa waendeshaji wa website hii..
Tumekusudia kukuhudumia kama mfalme! Tafadhali weka maoni yako kuhusu mtandao huu; tumeazimia kuufanya mtandao mmoja kwa ajili ya mahitaji yote, kama umepata tatizo la udanganyaji au bidhaa feki au jengine lolote usisite kutujulisha moja kwa moja kupitia Mail Us au namba 0655 063 601 ili tuweze kulishughulikia haraka sana
Weka maoni yako
Email yako haitawekwa wazi, maelezo yanayohitajika yamewekwa alama ya *
Maksi zako