MAMBO SABA WANAYOYAFANYA MASKINI, AMBAYO MATAJIRI HAWAYAFANYI
Maelezo
Chanzo: Zenjishoppazz
Tarehe Iliyotolewa: 2022-12-18
MAMBO 7 WANAYOYAFANYA MASKINI, AMBAYO MATAJIRI HAWAYAFANYI
Je, unataka kuwa tajiri? Je, ni baadhi ya mambo yapi ambayo watu maskini hufanya ambayo yanazuia maendeleo yao? Dan anafichua baadhi ya mambo na tabia zinazowafanya watu kuendelea kuwa maskini. Ni mambo gani saba masikini, wanafanya ambayo matajiri hawafanyi.
Maskini Wanatazama TV sana, wakati Matajiri Wanasoma Vitabu sana
Watu waliofanikiwa zaidi ulimwenguni huutumia muda wao mwingi katika kusoma vitabu na si kwa kutazama TV. Kwa mfano Warren Buffett (mtu wa nne tajiri zaidi duniani), husoma kurasa Zaidi ya 500 za vitabu kila siku. Na hii humsaidia kupata ujuzi na maarifa mapya kila siku.
Ili na wewe kufanikiwa Zaidi inapasa kusoma vitabu iwezekanavyo. Kwa hivyo, itupe TV yako nje ya dirisha, chukua kitabu ambacho kitakuboresha wewe binafsi, na uanze kusoma kila siku kwani vitakupa ujuzi na maarifa mapya kila siku.
Maskini hulipwa Kulingana Na Wakati, wakati Matajiri Hulipwa Kulingana na Matokeo
Ni muhimu kutambua kwamba matokezeo ni thamani halisi ya ulimwengu, hili ni jambo la kushangaza. Haijalishi kama wewe ni bora katika kazi yako unayoifanya. Utaonekana kama watu wengine wa kawaida ikiwa huchangii katika jambo kubwa Zaidi, kama wajasiraia mali wanavyofanya. Usiogope kufanya jambo kubwa ambalo litaleta, ambalo litamshitua kila mtu, na kubadilisha ulimwengu kwa ujumla kama alivyofanya Elon Musk.
Maskini Hupenda kulalamika sana wakati Matajiri huwajibika.
Usikubali kuingia katika mtego wa kulaumu. Kulaumu mazingira ya nje, kama vile kulaumu watu wengine kunaondosha nguvu zako, Haijalishi changamoto unazokabiliana nazo, ni jukumu lako kukabiliana nazo na kuzibadilisha kutoka changamoto kuwa fursa. Matajiri hujiamini, kwa kujua maisha yao yako mikononi mwao wenyewe. Ikiwa unataka kufanikiwa Zaidi na zaidi, jitahidi kufanya vizuri Zaidi na uache kulaumu; na uanze kufanya yaliyobora zaidi.
Watu Maskini Wanazingatia Kuweka Akiba | Matajiri Wanazingatia Uwekezaji
Kama Dan Lok alivyosema, “huna tatizo la kueka akiba, una tatizo la kipato. Hivyo kuweka akiba ni jambo muhimu kwa ajili ya kuweza kupata mafanikio na kuweza kujiwekeza zaidi
Zinazofanana
- Ajali ya MV Spice Islander
- Ifahamu Museum for the Future Dubai
- Matokeo ya Kidato cha Nne (Form Four) 2022/2023
- The Motivation Myth
- TABIA 12 ZA MATAJIRI/MAMILIONEA
- Mambo saba ya kujifunza katika kitabu cha The Richest Man in the Babylon
- History Form One Notes
- KARIBU USAFIRI NASI KWA SAFARI YA HIJA
- NAMNA NZURI YA KUWEZA KUHIFADHI PESA