AFISA TATHMINI NA USAJILI BIDHAA ZA CHAKULA DARAJA LA II-UNGUJA - 1 POST

Maelezo

Chanzo: zan ajira



Tarehe Iliyotolewa: 2025-08-16



Kituo cha Kazi/Tukio: Unguja
Imetembelewa mara! 801 ... Deadline: 2025-08-30 15:30:00

POST DETAILS

POSTAFISA TATHMINI NA USAJILI BIDHAA ZA CHAKULA DARAJA LA II-UNGUJA - 1 POST
EMPLOYERZANZIBAR FOOD AND DRUG AGENCY (ZFDA)
APPLICATION TIMELINE:From: 16-08-2025 To: 30-08-2025
DUTIES AND RESPONSIBILITIES

Majukumu

  1. Kusaidia kukagua na kutathmini nyaraka zilizowasilishwa kama sehemu ya maombi ya usajili wa bidhaa za chakula;
  2. Kusaidia kutathmini maombi ya usajili wa bidhaa za chakula kwa kuhakikisha ukamilifu wake na kufuatwa kwa vigezo vilivyowekwa;
  3. Kusaidia uchambuzi na tathmini ya nyenzo za matangazo yanayohusiana na bidhaa za chakula ili kuhakikisha kuwa yanakwenda sambamba na vigezo vya udhibiti;
  4. Kuandaa ripoti za tathmini za kina na ripoti za maendeleo na kuziwasilisha kwa mkuu wa Divisheni;
  5. Kuhuisha hifadhidata ya usajili wa bidhaa za chakula kwa taarifa sahihi na zinakwenda na wakati;
  6. Kushughulikia na kujibu maswali ya wateja yanayohusiana na usajili wa bidhaa za chakula, kwa kutoa taarifa na msaada inapohitajika;
  7. Kushiriki katika kampeni za uhamasishaji wa umma kuhusu usalama wa chakula na umuhimu wa bidhaa zilizojisajili;
  8. Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka; na
  9. Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE

Sifa za Muombaji:

  • Awe ni Mzanzibari.
  • Awe amehitimu shahada ya kwanza katika fani ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia (Food Science and Technology) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
  • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.
REMUNERATIONZPSH-10



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2025 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English