NAMNA NZURI YA KUWEZA KUHIFADHI PESA

Maelezo

Chanzo: Zenjishoppazz



Tarehe Iliyotolewa: 2022-12-11



Kituo cha Kazi/Tukio: Zanzibar
Imetembelewa mara! 22584 ... Deadline: 2027-12-31 06:38:00

Je una lengo kwa mwaka 2023 la kuhifadhi pesa Zaidi katika akaunti yako ya benki au nyumbani?

Kama jibu lako ni ndio, basi hongera na karibu sana tukupe somo ambalo litakusaidia sana katika kuhifadhi pesa.

Ili kuweza kukusaidia kuhifadhi pesa zako ambazo zitakusaidia katika kufungua biashara au kuweza kujiajiri kinyume na kazi yako ya kudumu basi jaribu kumshirikisha mkeo katika kuhifadhi pesa zako huenda ukafanikiwa.

Andaa daftari lako au notebook au hata diary ambayo utakua ukiandika matumizi yako ya kila siku, wiki, na hata mwezi.

Jambo hili litakusaidia kujua kila pesa wapi ilipotumika na hivyo itakusaidia kuweza kujua sehemu gani katika matumizi yako unatumia Zaidi.

Hakikisha unaandika kila kitu kuanzia kipato unachokipata Pamoja na matumizi yake kama vile kodi ya nyumba, umeme, maji nk.

Katika kile unachokipata hakikisha unaeka asilimia 20 ya kipato chako kama akiba ya kila mwezi.

Na vile vile kwa kugawa matumizi ya lazima na yale ambayo sio ya lazima kwa jambo hii itakusaidia kujua wapi uweke pesa nyingi na wapi upunguze matumizi.

Na namna ya mwisho ni kwa kugawa pesa katika bahasha, ambapo pesa hizo utazitia katika bahasha na kila bahasha utaandika juu yake kama vile matumizi ya lazima ikiwemo kula, kodi na bili.

Na yasiyo ya lazima kama vile mavazi na kuwatowa Watoto out, na matumizi ya ziada kama vile kuwapa wengine zawadi na hata msaada. 

Hivyo lazima ujieekee mkakati wa kuwa usitowe pesa katika bahasha nyengine hata kama zitaisha maana yake inabidi zisubiri bajeni ya mwezi mwengine.

Ukiwa utafanya hivi juwa utaweza kujiekea akiba ya kutosha na hata kufanikiwa kwa kufungua biashara nyengine nje ya ajira yako uliyoajiriwa. Ila itakubidi ueweze kujilazimisha na kuifosi nafsi katika utekelezaji wake.

Kama ukifanya hivi hadi kufika mwishoni mwa 2023 basi utakuwa na akiba ya kutosha kwa ajili ya kujiwekeza.



Share via Whatsapp
Advertise with us

©2024 Zenji Shoppazz . Haki zote zimehifadhiwa | Imetengenezwa na W3layouts and Zenji Shoppazz Chagua lugha : English